28 Aprili 2025 - 22:45
Source: Parstoday
Araghchi: Kuendelea kuzingirwa Gaza na kuuawa watu wasio na hatia ni jinai isiyo na mfano

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, kuendelea kuzingirwa Gaza na kuuawa watu wasio na hatia ni jinai isiyo na mfano katika historia ya mwanadamu.

Sayyid Abbas Araghchi amesema hayo katika mazungumzo yake kwa njia ya simu na Badr Abdulatti, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Misri na kubainisha kwamba, kuendelea kuzingirwa Gaza na kutoingizwa chakula na dawa, na mauaji ya watu wasio na hatia ni jinai isiyo na mfano wake katika historia ya mwanadamu.

Aidha amesema, Marekani na waungaji mkono wengine wa utawala wa Kizayuni wa Israel ni washirika wa jinai ya mauaji ya mauaji kimbari na jinai za vita zinazofanywa na Israel huko Palestina.

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran amesisitiza ulazima wa kukabiliana na siasa za utawala wa Kizayuni katika kuwatimua watu wa Gaza na Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na kueleza upuuzaji wa jamii ya kimataifa dhidi ya jinai hizo kuwa ni jambo la kushangaza na la kutia wasiwasi.

gaaza

Araghchi: Kuendelea kuzingirwa Gaza na kuuawa watu wasio na hatia ni jinai isiyo na mfano

Muonekano wa Gaza

Katika mazungumzo hayo, Araghchi amemueleza pia waziri mwenzake wa Misri kuhusiana na hatua zilizopigwa katika mazungumzo yasiyo ya ana kwa ana ya Marekani na Iran.

Kwa upande Badr Abdulatti, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Misri ametoa mkono wa pole kwa taifa la Iran kufuatia mlipuko katika Bandari ya Shaheed Rajaei, na kuwatakia ahueni ya haraka majeruhi wa ajali hiyo.

Badr Abdulatti ameashiria pia juhudi zinazoendelea za Misri za kusimamisha jinai za utawala wa Kizayuni katika Palestina inayokaliwa kwa mabavu na kutoa msaada kwa watu waliokimbia makazi yao huko Gaza, na kumfahamisha mwenzake wa Iran kuhusu matukio ya hivi karibuni kuhusiana na suala hili.

Your Comment

You are replying to: .
captcha