29 Aprili 2025 - 19:36
"Fatima Masuma (a.s), Kielelezo cha Mwanamke Mwadilifu" | Sherehe Yafana Katika Shule ya Wasichana ya Hazrat Zainab (s.a), Kigamboni, Picha + Video

Leo, katika shule ya wasichana, hafla ya kuadhimisha siku ya kuzaliwa kwa Bibi Mtakatifu, Hadhrat Fatima Maasumah (s.a) imefanyika kwa mafanikio makubwa katika Shule ya Wasichana ya Hadhrat Zainab (s.a), iliyopo Kigamboni Jijini Dar-es-Salam - Tanzania.

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) - ABNA - Katika mnasaba wa Hafla ya Kuzaliwa kwa Sayyidat Fatima Maasumah (s.a), Wanafunzi na Walimu walipata fursa ya kufaidika na hotuba maalumu iliyotolewa na Mrs.Taqavi, Mudir, Msimamizi na Kiongozi Mkuu wa shule hiyo ya Wasichana ya Hadhrat Zainab (s.a). Hotuba yake iligusa nyoyo za wasikilizaji kwa kuangazia maisha, nafasi na sifa tukufu za Bibi Fatima Maasumah (s.a) katika historia ya Uislamu, pamoja na nafasi ya Mwanamke katika Jamii ya Kiislamu.

"Fatima Masuma (a.s), Kielelezo cha Mwanamke Mwadilifu" | Sherehe Yafana Katika Shule ya Wasichana ya Hazrat Zainab (s.a), Kigamboni, Picha + Video

Mrs.Taqavi, Msimamizi na Kiongozi Mkuu wa shule hiyo ya Wasichana ya Hadhrat Zainab (s.a) akizungumza mbele ya hadhira iliyojawa na shauku, alisema:

"Bibi Fatima Masuma (a.s) alikuwa kielelezo cha maarifa, uchamungu, na ujasiri wa mwanamke Mwislamu. Kumbukumbu yake ni fursa ya kutafakari nafasi ya mwanamke katika kusimamisha dini na jamii yenye maadili."

"Fatima Masuma (a.s), Kielelezo cha Mwanamke Mwadilifu" | Sherehe Yafana Katika Shule ya Wasichana ya Hazrat Zainab (s.a), Kigamboni, Picha + Video

Wanafunzi walifurahia sana maudhui ya hotuba hiyo, huku wengi wao wakichukua nukta muhimu kwa ajili ya kumbukumbu zao kuhusiana na maisha, fadhila na mwenendo wa Sayyidat Fatima Maasumah (s.a). Hafla hiyo ilijaa hali ya kiroho, hamasa na hali ya kujifunza zaidi, huku wanafunzi wakionyesha furaha yao kwa kushiriki katika hafla hiyo kumbukumbu hiyo tukufu. Shughuli mbalimbali za kiroho pia zilifanyika, zikiwemo kaswida, na mawaidha mafupi kutoka kwa walimu. 

"Fatima Masuma (a.s), Kielelezo cha Mwanamke Mwadilifu" | Sherehe Yafana Katika Shule ya Wasichana ya Hazrat Zainab (s.a), Kigamboni, Picha + Video

 Tizama picha zaidi za Tukio hili hapa chini

Your Comment

You are replying to: .
captcha