29 Aprili 2025 - 19:59
Source: Parstoday
Mbunge wa Marekani awasilisha ibara saba za hoja za kumsaili Trump kwa lengo la kumuuzulu

Mbunge wa chama cha Democrat katika Bunge la Marekani Shri Thanedar amewasilisha vifungu saba vya hoja ya kumsaili na kumuuzulu rais wa nchi hiyo Donald Trump.

Thanedar, anayewakilisha jimbo la Michigan, amezitaja sababu za kutaka Trump asailiwe na kuuzuliwa kuwa ni "matumizi mabaya kupindukia ya madaraka, ukiukaji wa wazi wa Katiba, na vitendo vya kidhalimu ambavyo vinadhoofisha demokrasia ya Marekani na kutishia utawala wa sheria."

"Donald Trump ameonyesha mara kwa mara kwamba hafai kuhudumu kama rais na ni kielelezo cha hatari ya wazi na iliyopo kwa katiba ya taifa letu na demokrasia yetu," ameeleza Thanedar katika taarifa aliyotoa jana Jumatatu.

Katika taarifa yake hiyo, mbunge huyo wa chama cha Democrat ameendelea kusema: "vitendo haramu vya Trump vimeharibu mfumo wa haki, kukiuka mgawanyo wa mamlaka, na kuweka mamlaka ya binafsi na maslahi binafsi juu ya utumishi wa umma. Hatuwezi kusubiri ufanywe uharibifu zaidi. Lazima Bunge lichukue hatua".

Rais huyo wa Marekani leo atakuweko kwenye jimbo la Michigan kusherehekea siku 100 za muhula wake wa pili wa kuweko madarakani.../

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha