29 Aprili 2025 - 15:56
Hafla ya Kuzaliwa kwa Hadhrat Bibi Fatima Maasumah (s.a) Yafanyika katika Madrasat ya Imam Zain Al-A'bidin (a.s), nchini Burundi + Picha

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) - ABNA - Madrasa ya Imam Zain al-A'bidin (a.s) nchini Burundi imefanikiwa kuandaa hafla adhimu ya kuadhimisha kuzaliwa kwa Hadhrat Bibi Fatima Maasumah (s.a), mmoja wa Wanawake Mashuhuri na wenye nafasi ya kipekee katika Historia ya Uislamu. Mada kuu ya maadhimisho haya ilikuwa: "Jukumu la Kielimu la Wanawake katika Uislamu na Athari Yao katika Maendeleo ya Utamaduni wa Kiislamu."

Tukio hili lililofanyika kwa heshima ya Bi Fatima MaasumaH (S.A) limehudhuriwa na Waumini wa rika mbalimbali, hususan Wanawake na Wasichana kutoka maeneo tofauti. Mada kuu ya maadhimisho haya ilikuwa: "Jukumu la Kielimu la Wanawake katika Uislamu na Athari Yao katika Maendeleo ya Utamaduni wa Kiislamu."

Hafla ya Kuzaliwa kwa Hadhrat Bibi Fatima Maasumah (s.a) Yafanyika katika Madrasat ya Imam Zain Al-A'bidin (a.s), nchini Burundi + Picha

Katika hotuba mbalimbali zilizotolewa, wahadhiri walisisitiza nafasi ya juu ya wanawake katika elimu na malezi ya jamii, wakimnukuu Bibi Fatima Maasumah (s.a) kama mfano wa Elimu, Ucha Mungu, na kujitolea kwa ajili ya Uislamu. Aidha, walisema kuwa historia ya Kiislamu imejaa Wanawake waliotoa mchango mkubwa katika kutunza misingi ya dini na kueneza maadili ya Kiislamu.

Kwa upande wake, viongozi wa madrasa hii walitoa wito kwa Wanawake wa Kiislamu kuendelea kujielimisha na kushiriki kikamilifu katika kuendeleza jamii zao kwa msingi wa elimu, maadili mema, na upendo kwa Ahlulbayt (a.s.).

Hafla hiyo ilipambwa na burudani za kiroho, qaswida, mashairi ya kuenzi kizazi cha Mtume (s.a.w.w), pamoja na dua maalum kwa ajili ya umoja wa Waislamu na ushindi wa Waislamu katika maeneo mbalimbali duniani.

Kwa mara nyingine, Madrasa ya Imam Zain al-A'bidin (a.s.) nchini Burundi, imeonesha dhamira yake ya kukuza elimu na kuinua hadhi ya Wanawake katika jamii kwa kuegemea katika mwanga wa mafundisho ya Ahlulbayt (a.s.).

Your Comment

You are replying to: .
captcha