Awamu ya nne na ya mwisho wa uchaguzi wa manispaa na serikali za mitaa katika majimbo ya kusini mwa Lebanon na Nabatieh, ilifanyika jana Jumamosi Mei 24, 2025 katika anga ya utulivu na huru na kumalizika kwa ushindi mkubwa na mutlaki wa mrengo unaounga mkono Hizbullah.
Ushindi huo mkubwa wa kambi ya Muqawama umepatikana katika hali ambayo baadhi ya makundi ya vibaraka wa Magharibi yalikuwa na hamu ya kuona Muqawama unakosa kura, ili yapate fursa ya kudai kuwa umaarufu wa Hizbullah umepungua.
Zoezi la kupiga kura lilianza saa moja asubuhi jana Jumamosi na kuendelea hadi saa moja usiku. Mara baada ya kumalizika kupiga kura, lilianza zoezi la kuhesabu kura. Baadaye Wizara ya Mambo ya Ndani ya Lebanon ikatangaza ushindi mutlaki wa kambi ya Muqawama ikiongozwa na Hizbullah.
Kwa mujibu wa Tume ya Uchaguzi ya Hizbullah, wagombea wa mrengo wa Muqawama walipita bila ya kupingwa katika viti 102 kati ya 272 vya manispaa za miji. Ni katika eneo la Hasbaiyya pekee ndiko kulikofanyika uchaguzi kwa mchuano baina ya wagombea wa mirengo tofauti na pamoja na hayo, mrengo wa Muqawama umepata ushindi.
342/
Your Comment