18 Juni 2025 - 16:20
Video | Vituo vyote vya kidini Afghanistan vimeombwa kuombea ushindi wa Iran + Video

“Katika wakati huu wa majaribu makubwa, tunawaomba waumini na viongozi wa dini kote Afghanistan kuunganisha dua na ibada kwa ajili ya ushindi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran dhidi ya utawala dhalimu wa Kizayuni. Ushindi huu ni ushindi wa haki dhidi ya dhulma, na ni wajibu wa kila muumini kumuombea ndugu yake katika dini.”

Shirika la Habari la Kimataifa AhlulBayt (as) -ABNA- Hujjatul Islam wal Muslimin, Ustad Akhlaqi, Imamu wa Ijumaa wa Waislamu wa Kishia katika mkoa wa Bamyan na mkuu wa ofisi ya Ayatullah al-Udhma Muhhaqiq Kabuli (r.a) katika mji huo, ametuma ujumbe kwa shirika la habari la ABNA akitoa wito kwa waumini na vituo vyote vya kidini nchini Afghanistan kuwaombea ushindi Waislamu wa Iran dhidi ya adui Mzayuni.

Video | Vituo vyote vya kidini Afghanistan vimeombwa kuombea ushindi wa Iran + Video

Katika ujumbe wake, amesema:
“Katika wakati huu wa majaribu makubwa, tunawaomba waumini na viongozi wa dini kote Afghanistan kuunganisha dua na ibada kwa ajili ya ushindi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran dhidi ya utawala dhalimu wa Kizayuni. Ushindi huu ni ushindi wa haki dhidi ya dhulma, na ni wajibu wa kila muumini kumuombea ndugu yake katika dini.”

Amesisitiza kuwa mshikamano wa kimataifa wa Waislamu na watu wa haki ni silaha kubwa katika kukabiliana na maadui wa Uislamu na ubinadamu.

Your Comment

You are replying to: .
captcha