21 Juni 2025 - 13:04
Source: IQNA
Wasomi wa Kiislamu Palestina waunga mkono Iran

Baraza la Maulamaa wa Kiislamu Palestina limetoa taarifa na kutangaza kufungamana na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika kukabiliana na utawala wa Kizayuni wa Israel.

Sheikh Hussein Qassem, mkuu wa Baraza la Maulamaa wa Kiislamu Palestina ametoa taarifa akitangaza kufungamana na  na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

“Sisisote tunasimama kwa ushujaa na heshima pamoja na Iran ya Kiislamu katika kukabiliana na mashambulizi ya utawala wa kijinai wa Israel. Iran, kwa uwezo wake Mwenyezi Mungu, itapata ushindi   dhidi ya utawala wa Israel wenye kiu cha damu na utendao jinai, utawala ambao ni muuaji wa wanawake na watoto, ni adui wa haki, dini, ubinadamu elimu na maadili.”

Aidha Sheikh Muhammad Saleh al Muaid, msemaji rasmi wa baraza hilo naye amesema: “Sote tuko pamoja na Iran, nchi ambayo inalinda heshima, hadhi, dini, umoja na utamaduni wa vizazi vijavyo vya ummah wa Kiislamu.”

Amelaani pia kimya cha nchi za Kiarabu mbele ya kiburi cha utawala wa Kizayuni.

Akizihutubu tawala hizo za Kiarabu, Sheikh Al Muaid amesema: “Ni aibu kuwa baadhi ya Waislamu wamesalia kimya kwa miaka miwili mbele ya jinai ya mauaji ya kimbari inayotekelezwa na Israel huko Gaza.”

Ameonya kuwa, vita vilivyoanzishwa na utawala haramu wa Isarel vinalenga kuangamiza Iran, Palestina na eneo zima na hivyo tuko katika wakati muhimu sana. “Wote wanapaswa kufahamu kuwa katika uadui huu ulioanzishwa, kila mtu analengwa kwani bila shaka vitaainisha hatima ya eneo na vizazi vijavyo katika miaka mingi ijayo.’

Ametoa wito kwa Waislamu kuungana na kuunga mkono Iran na kusimama pamoja nayo kwani Iran leo inatetea hatima ya eneo lote.

Sheikh al Muaid amesisitiz akuwa: “Ukweli hatimaye utashinda kwani Iran, katika vita dhidi ya adui Mzayuni, inawakilisha haki na Uislamu na inatetea heshima ya ummah wote wa Kiislamu. Batili, ambayo dhihirisho lake ni Shetani, adui Mzayuni, Marekani, madola yote dhalimu ya Magharibi, na Waarabu wenye woga ambao wametupa heshima yao na kuacha watu wa Haza wachinjwe, kwa uwezo wake Mwenyezi Mungu watashindwa.

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha