21 Juni 2025 - 13:07
Source: IQNA
Msomi wa Morocco: Nchi za Kiislamu ziunge mkono Iran kukabiliana na hujuma ya Israel

Rais wa zamani wa Jumuiya ya Kimataifa ya Maulamaa Waislamu, Sheikh Ahmed al Raissouni, ametoa wito kwa Waislamu duniani kote kuunga mkono Iran katika kukabiliana na hujuma ya kijeshi ya utawala wa Kizayuni wa Israel, huku akisisitiza kuwa hakuna taifa ambalo limewaunga mkono ukombozi wa Palestina kama ilivyofanya Iran.

Msomi huyo maarufu wa Morocco amesema ni wakibu kwa Waislamu wote kuunga mkono Iran kukabiliana na vitendo vya uchokozi vya utawala haramu wa Israel.

“Tokea ulipoundwa utawala haramu wa Kizayuni wa Israel, hakuna nchi yoyote imejitolea na kufungamana na kadhia ya ukombozi wa Palestina kama ilivyofanya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran,”  amesema Sheikh Raissouni. “Hakuna nchi yoyote ya Kiarabu au ya Kiislamu imeweza kuwasaidia Wapalestina kama ilivyofanya Iran, hata ujijumuisha msaada wa nchi hizo zote.”

Sheikh Raissouni ambaye  ni msomi maarufu wa Kisunni ambaye alichukua mahala pa Sheikh Yusuf al Qaradawi kama mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Maulamaa Waislamu, amesema kuwa, kutetea msimamo wa Iran ni wajibu wa kidini na kimaadili kutokana na uungaji mkono wake wa miongo kadhaa wa mapambano ya ukombozi wa Palestina.

Utawala wa Kizayuni wa Israel ulianzisha uchokozi dhidi ya Iran Juni 13 kwa kutekeleza mashambulizi ya angani dhidi ya meneo ya kiraia na kijeshi. Makamanda wa ngazi za juu wa kijeshi pamoja na wanasayansi wa nyuklia na idadi kubwa ya  raia, hasa wanawake na watoto wameuawa katika hujuma hiyo ya Israel.

Katika kujibu uchokozi huo,  Iran ilianzisha operesheni yakijeshi iliyopewa jina ya Ahadi ya Kweli III, ambapo hadi sasa imevurumisha mamia ya makombora na ndege za kivita zisizo na rubani dhidi ya Israel na kulenga vituo vya kijeshi na kijasusi vya utawala huo dhalimu.

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha