Ofisi ya Ayatullah Sistani imetoa taarifa Jumatano na kuonya kuwa jinai kama hiyo,mbali na kukiuka misingi ya kidini na kimaadili, ni ukiukaji wa wazi wa sheria za kimataifa na inaweza kuwa na matokeo mabaya kwa eneo zima. Aidha mwanazuoni huyo amesema jinai kama hizo zinaweza kuepelekea hali iwe mbaya zaidi na kuongeza masaibu ya watu wa eneo na kuhatarisha maslahi ya kila mtu.
Aidha mwanazuoni huyo wa Iraq ametoa wito kwa taasisi za kimataifa na serikali za dunia, hasa za nchi za Kiislamu, kuchukua hatua za kumaliza vita hivi vya kidhalimu vilivyoanzishwa na Israel na kutafuta suluhu ya kudumu na ya haki kuhusu kadhia ya nyuklia ya Iran kwa mujibu wa sheria za kimataifa.
Utawala wa Kizayuni wa Israel ulianzisha uchokozi dhidi ya Iran Juni 13 kwa kutekeleza mashambulizi ya angani dhidi ya meneo ya kiraia na kijeshi.
Katika kujibu uchokozi huo, Iran ilianzisha operesheni yakijeshi iliyopewa jina ya Ahadi ya Kweli III, ambapo hadi sasa imevurumisha mamia ya makombora na ndege za kivita zisizo na rubani dhidi ya Israel na kulenga vituo vya kijeshi na kijasusi vya utawala huo dhalimu.
342/
Your Comment