26 Juni 2025 - 23:05
🚩Huyu Ndiye Imam Hussein (as) na hawa ndio Wafuasi na Wapenzi wa Imam Hussein(as) - Mjukuu wa Mtume wetu Muhammad (saww) + Video

Imam Hussein (as), alikuwa mja Mwema wa Allah, na Yazidi na watu wake, na Wafuasi wake kokote walipo Duniani na kila zama, ni kundi la waovu na ni watu wa upande wa batili. Na Hapana Shaka kuwa Moto wa Jahannam umeandaliwa kwa ajili ya watu waovu na Wafuasi wa wa waovu na walaaniwa Duniani na Akhera, ambao walishiriki moja kwa moja au kwa Njia isiyokuwa ya moja kwa moja katika kukiua na kukichinja Kizazi Kitukufu cha Mtume wetu Muhammad (saww). Hao makazi mafikio yao na makazi yao ya milele ni Jahannam (Khalidina Fiha Abada).

Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Video hii inaonyesha Wafuasi na Wapenzi wa Imam Hussein (as), Shujaa na Mjukuu wa Mtume Muhammad (saww), wakiwa katika hali ya kuupokea Mwezi wa Huzuni, Mwezi wa Muharram ambao ndani yake aliuliwa kinyama Mjukuu wa Mtume wetu Muhammad (saww), kupitia mikono ya waovu wa Kizazi kiovu cha Bani Umaiyya, wakiongozwa na Mlaaniwa Yazid bin Muawiya.

🚩Huyu Ndiye Imam Hussein (as) na hawa ndio Wafuasi na Wapenzi wa Imam Hussein(as) - Mjukuu wa Mtume wetu Muhammad (saww) + Video

Imam Hussein (as), alikuwa mja Mwema wa Allah, na Yazidi na watu wake, na Wafuasi wake kokote walipo Duniani na kila zama, ni kundi la waovu na ni watu wa upande wa batili.

Na Hapana Shaka kuwa Moto wa Jahannam umeandaliwa kwa ajili ya watu waovu na Wafuasi wa wa waovu na walaaniwa Duniani na Akhera, ambao walishiriki moja kwa moja au kwa Njia isiyokuwa ya moja kwa moja katika kukiua na kukichinja Kizazi Kitukufu cha Mtume wetu Muhammad (saww). Hao makazi mafikio yao na makazi yao ya milele ni Jahannam (Khalidina Fiha Abada).

🚩Huyu Ndiye Imam Hussein (as) na hawa ndio Wafuasi na Wapenzi wa Imam Hussein(as) - Mjukuu wa Mtume wetu Muhammad (saww) + Video

Imam Hussein (as) alikubali damu yake imwagwe lakini Uislamu ubakie kuwa hai... Aliyekataa Kizazi kiovu cha Bani Umaiyya kuuchafua Uislamu na kuufyekelea mbali ... Mpaka akasema:

"Ikiwa Dini ya Muhammad haiwezi kuendelea kuwa hai na kusimama kwa uthabiti ispokuwa mpaka damu yangu imwagike, basi niko tayari enyi panga (za maadui) nichukueni"

🚩Huyu Ndiye Imam Hussein (as) na hawa ndio Wafuasi na Wapenzi wa Imam Hussein(as) - Mjukuu wa Mtume wetu Muhammad (saww) + Video

Wafuasi na Wapenzi wote wa Ahlul-Bayt - Kizazi Kitukufu cha Mtume Muhammad (amani iwe juu yao) -  hivi sasa wanaingia katika Mwezi Mtukufu wa Muharram ambao kwao ni Mwezi wa kuomboleza Shahada ya Imam wao, Kiongozi wao, Khalifa wao wa 3 Kati ya Makhalifa 12 (as), si mwingine bali ni Imam Hussein (as), Mjukuu Kipenzi wa Mtume wa Umma wa Kiislamu, Muhammad (saww).

Your Comment

You are replying to: .
captcha