26 Juni 2025 - 17:51
Siri yafichuka: Mahusiano ya Israel na Viongozi wa sasa wa Serikali ya mpito ya Syria

Mazungumzo ya moja kwa moja kati ya Syria na utawala haram wa Kizayuni (Israel) ni jambo ambalo kwa muda mrefu limeonekana kama hali isiyowezekana kutokana na migogoro ya kihistoria na migawanyiko ya kisiasa.

Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (as) - ABNA- Habari za Mahusiano ya sasa ya Syria na Israel ni za kushtua na zinaonyesha mabadiliko makubwa katika siasa za eneo la Mashariki ya Kati. 

Siri yafichuka: Mahusiano ya Israel na Viongozi wa sasa wa Serikali ya mpito ya Syria

Mazungumzo ya moja kwa moja kati ya Syria na utawala haram wa Kizayuni (Israel) ni jambo ambalo kwa muda mrefu limeonekana kama hali isiyowezekana kutokana na migogoro ya kihistoria na migawanyiko ya kisiasa.

Kufichuliwa kwa kiongozi wa Baraza la Usalama wa Taifa wa Israel, Tzachi Hanegbi, kwamba yeye ni mwakilishi wa mazungumzo haya, na kwamba Syria na Lebanon wanahusishwa kama wagombea wa kujiunga na mikataba ya amani kama mikataba ya Abraham, ni ishara ya kwamba kuna mabadiliko makubwa yanayojitokeza baada ya vikao hivyo vya kujiunga na mikataba hiyo ya Abraham ambayo ni mikitaba ya kuisaliti Quds na Palestina kwa ujumla.

Pia, kauli yake kuhusu uwezekano wa kuondoa majeshi ya Israel kutoka mpakani na Syria ikiwa uhusiano wa kawaida utaanzishwa ni hatua kubwa ya kidiplomasia, inayoweza kuleta mabadiliko pengine ya usalama na utulivu katika eneo hilo huku Palestina ikiendelea kuzingirwa na kukandamizwa na Utawala huo haram wa Israel kwa Msaada wa Nchi ya Syria inayoelekea kuwa sehemu ya vibaraka wa Israel.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha