Kwa mujibu wa shirika la habari la ABNA likinukuu shirika la habari la Al-Mayadeen, Wizara ya Mambo ya Nje ya Ufaransa leo Jumamosi imetoa taarifa ikisema: "Paris inalaani shambulio la Israel lililosababisha kujeruhiwa kwa askari wa UNIFIL kusini mwa Lebanon."
Hii ni wakati ambapo awali iliripotiwa kuwa milio mikali ya risasi kutoka kwa bunduki nzito za rashasha kutoka kwenye ngome za jeshi la uvamizi la Kizayuni kusini mwa "Blue Line", ililenga eneo la operesheni la doria ya UNIFIL iliyokuwa ikikagua kituo cha ukaguzi katika kijiji cha "Bastara".
Kwa upande mwingine, Kikosi cha Mpito cha Umoja wa Mataifa nchini Lebanon (UNIFIL) kimetangaza kuwa jeshi la utawala wa Kizayuni lilifyatua risasi kwa kutumia silaha za kiotomatiki karibu na doria mbili za kikosi hicho kusini mwa Lebanon. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, tukio hilo lilitokea baada ya mlipuko wa guruneti la mkono katika eneo la karibu, ambalo kufuatia hilo, mmoja wa askari wa UNIFIL alijeruhiwa.
Kufuatia hatua hiyo ya Tel Aviv, UNIFIL imetoa wito tena kwa Israel "kukomesha tabia zake za uchokozi".
Your Comment