4 Januari 2026 - 08:10
Source: ABNA
Trump: Baada ya Maduro, Marekani itaitawala Venezuela

Donald Trump wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari alisema: "Baada ya Maduro, Marekani itaitawala Venezuela."

Kwa mujibu wa shirika la habari la ABNA kupitia NPR, hotuba ya Donald Trump kuhusu uchokozi wa kijeshi dhidi ya Venezuela imeanza. Rais wa Marekani akielezea maelezo ya shambulio hilo alisema: "Kabla ya kushambulia makazi ya Maduro, tulikata umeme katika mji wa Caracas. Tuko tayari kwa shambulio kubwa zaidi; shambulio la kwanza lilifanikiwa. Lengo lilikuwa kumkamata Maduro na mkewe ili wafikishwe mahakamani."

Aliendelea: "Maduro alikamatwa usiku wa giza. Tulelemaza nguvu za kijeshi za Venezuela. Tunakusudia kuitawala Venezuela hadi hapo kutakapokuwa na mpito salama wa madaraka, na tutafanya uchaguzi. Makampuni ya mafuta ya Marekani yataenda Venezuela na kupata pesa."

Trump alikiri kuwa kuingilia kati kwa Marekani kutafungua milango mipya kwa makampuni ya mafuta ya Marekani. Kuhusu kiongozi wa upinzani Maria Corina Machado, alisema: "Ni vigumu kwake kuwa kiongozi. Hana uungaji mkono wala heshima ndani ya nchi."

Your Comment

You are replying to: .
captcha