Qur'an Tukufu haikuweka wazi hukumu ya kujenga juu ya makaburi; isipokua inawezekana kuifahamu hukumu yake kwa kupitia baadhi ya aya tukufu ambazo zimelizungumzia jambo hili kiujumla.
Hebu fuatilia ufafanuzi ufuatao:
1)KUJENGA JUU YA MAKABURI YA MAWALII NA KUVIHESHIMU VITU VITUKUFU VYA MWENYEZI MUNGU.
Hakika Qur'an Tukufu inakichukulia kitendo cha kuheshimu mambo matukufu ya Mwenyezi Mungu kua ni dalili ya utawa.
Mwenyezi Mungu anasema:
"Na yeyote anayeziheshimu alama za Mwenyezi Mungu,basi kufanya hivyo ni miongoni mwa uchaji wa moyo".(Qur'an 22:32)
Sasa tunajiuliza:Ni ni maana ya "TAADHIM SHA'AIRILLAH"
Jawabu:
"Sha'air" ni tamko la wingi na umoja wake ni "sha'irah" nalo lina maana ya dalili na alama, na wala haikua makusudio ya Sha'air" ktk aya hii kua ni alama zinazothibitisha kuwepo kwa Mwenyezi Mungu.
Mshairi mmoja anasema:
"Ktk kila kitu kuna dalili inayojulisha kwamba Mwenyezi Mungu ni mmoja"
Kama ambavyo ni vema ifahamike kwamba hakuna yeyote anayesema:
"kukiheshimu kila kitu kilichoko ulimwenguni ni dalili ya ucha Mungu." bali makusudio ni kuziheshimu dalili(alama) za dini ya Mwenyezi Mungu.
Na maana hii ndio ambayo waisemayo wafasiri wa Qur'an ktk aya hii kwamba neno "SHA'AIRULLAH" maana yake ni vitambulisho vya dini ya Mwenyezi Mungu.

Na iwapo "SAFA" na MAR-WAH" na pia ngamia anayepelekwa Mina kwa ajili ya kuchinjwa ni miongoni mwa alama za dini ya Mwenyezi Mungu, basi siyo kwa sababu nyingine bali ni kwa kua ni vitambulisho vya dini tukufu na mpenzi wa Mwenyezi Mungu Nabii Ibrahim(a.s).
Na iwapo Muzdalifah huitwa "MASH'AR" hiyo ni kwasababu ipo miongoni mwa alama za dini ya Mwenyezi Mungu Mtukufu; na kwamba kusimama ktk Mash'ar hiyo ni dalili za kumtii Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Vile vile ibada za Hija zinapoitwa kua ni Sha'air, basi siyo kwasababu nyingine isipokua ni kwa kua ni alama za tauhidi na za dini tukufu. Kwa kifupi ni kwamba, kila kitambulisho cha dini ya Mwenyezi Mungu, kukiheshimu ni ktk mambo yanayomsogeza mtu ktk ucha Mungu.
Hivyo basi hakuna shaka kwamba Manabii na Mawali wa Mwenyezi Mungu, wao ndio alama kubwa zaidi miongoni mwa alama za Mwenyezi Mungu, kwani wao walikua ndio njia bora ya kufikisha ujumbe wa Mwenyezi Mungu na kuueneza miongoni mwa watu.