Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahl al-Bayt (A.S) - ABNA -, Ayatollah Al-Udhma "Hossein Nouri Hamedani" ambaye ni mmoja wa Marajii Taqlid wa Madhehebu ya Shia, ametoa ujumbe katika mkutano wa vyama (au jumuiya za) kisayansi za Seminari (Hawza) ya Qom kama ifuatavyo:
Kwa Jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu
الْحَمْدُ لِلَّهِ رَبِّ الْعَالَمِینَ وَالصَّلَاةُ وَالسَّلَامُ عَلَی سَیِّدِنا وَنَبِیِّنَا أَبِی الْقَاسِمِ المصطفی مُحَمَّد وَعَلَی أهلِ بَیتِهِ الطَّیِّبِینَ الطَّاهِرِینَ سیَّما بَقیَّهَ اللهِ فِی الأرَضینَ
Sifa zote njema ni za Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu wote, na rehema na amani ziwe juu ya Bwana wetu na Mtume wetu, Abu al-Qasim, Al-Mustafa (Mteule) Muhammad, na juu ya Familia yake wema na Watoharifu, Hasa kwa Baqiyyatullah -ambaye ni uthibitisho (Hojja) wa mwisho wa Allah uliobakia - ardhini.
«جاؤُا بِالْبَیِّناتِ وَ الزُّبُرِ وَ الْکِتابِ الْمُنِیرِ» آل عمران، ۱۸۴.
"Na wakikukanusha basi walikanushwa Mitume wengine kabla yako walio kuja na hoja waziwazi na Vitabu vyenye hikima, na Kitabu chenye nuru".
Salamu kwa Mkutano huo Mtukufu unaofanyika kwa kuhudhuriwa na Mafakihi na Wanasayansi wanaoheshimika.
Naipongeza Jumuiya yenu ya Wanafikra, Wasomi na Maprofesa na ninaichukulia kama ishara nzuri. Na Mwenyezi Mungu akipenda (Insha Allah) nyinyi waendelezaji wa njia ya Manabii (a.s) ambao siku zote walikuwa na dalili zilizo wazi, maandishi na vitabu vya kuelimisha.
Jamii za Kisayansi ni walinzi na ngome za mipaka ya fikra, kimbilio salama kwa fikra mpya na safi, na pia ni kimbilio la wale wenye nia na watafutaji ukweli na uhakika, na ni mti mzuri (nasaba njema) ya kujibu maswali mapya ya kidini ambayo yanatokana na urithi wa kudumu wa sayansi na mafundisho ya Uislamu na urithi wa Mtume wetu (rehema na amani ziwe juu yake na Aali zake).
Sasa, baada ya miongo miwili ya shughuli adhimu za jumuiya za kisayansi za Hawza, na hasa kwa maendeleo yaliyotokea katika kipindi cha hivi karibuni na maendeleo na ukuzaji ambao Alhamdulillah umeundwa (na kupatikana), inatarajiwa kwamba mkutano huu wa wanafikra na wenye maoni katika nyanja za sayansi za Binadamu na Sayansi za Kiislamu, kwa lengo la kuweka dhamira nzito ya kusimamisha Dini katika jamii, kwa maingiliano na watu na mfumo wa sasa wa Uislamu, utajitahidi zaidi kutoa njia ya kutatua matatizo ya sasa ya nchi.
Bila shaka, nuru ya Shule ya Mwangaza ya Ahlul-Bayt (amani iwe juu yao) imeangaza sehemu mbalimbali za dunia leo hii, ambayo imeelekeza akili za wanaotaka na kuamsha (kuzindua) asili (fitrah) kwenye bahari hii ya ujuzi na ufahamu, na kwa msingi huu, ni muhimu sana kwamba vyama vya kisayansi -Jumuiya za Kisayansi - vijipange kukabiliana na mahitaji haya ya Kisayansi Kimataifa na kwa ufanisi kwa kuwasiliana na ulimwengu wote, na kuchukua hatua za kivitendo katika kuanzisha na kuthabitisha mzunguko wa viti vya masomo ya kuujua Uislamu, Kuujua Ushia, na mafundisho na maisha bora ya Maasumin (amani iwe juu yao).
Pamoja na misheni na majukumu yote ya kitaifa na kimataifa, vyama vya kisayansi vina wajibu mzito kwa masuala ya elimu, utafiti, uboreshaji na uenezi wa seminari (hawza). Ni muhimu kuzingatia huduma na shughuli za jumuiya (za kisayansi) katika utekelezaji wa mifumo ya elimu ya wanafunzi katika ngazi ya Mapinduzi ya Kiislamu, uzalishaji na tathmini ya elimu ya kisasa, Matni (silabasi) za kisasa na kazi (athari za kiuandishi), hayo ni suala muhimu la Tablighi, Inapaswa kuzingatiwa kwa njia tofauti na siku za nyuma na kupata ufafanuzi mpya wa utambulisho na nafasi ya -jumuiya za kisayansi au - vyama vya kisayansi kuhusiana na vituo na Taasisi za Seminari (Hawza).
Mwisho, ningependa kuwathamini na kuwaheshimu nyinyi Wanasayansi katika Mkusanyiko huu mkubwa na kumwomba Mwenyezi Mungu kwa ajili ya mafanikio yenu ya zaidi pamoja na watumishi (wahudumu) wote wa Sayansi, Kiroho, Maadili na Sheria, pia ninashukuru na kkuthamini juhudi na jitihada za Mheshimiwa Mkurugenzi wa Seminari, juhudi za sekretarieti ya vyama vya kisayansi, na nguzo za kisayansi na mchango na uenzi wa vyama vyote vya kisayansi vya Hawza.
اللَّهُمَّ إِنَّا نَرْغَبُ إِلَیْکَ فِی دَوْلَةٍ کَرِیمَةٍ تُعِزُّ بِهَا الْإِسْلامَ وَ أَهْلَهُ وَ تُذِلُّ بِهَا النِّفَاقَ وَ أَهْلَهُ وَ تَجْعَلُنَا فِیهَا مِنَ الدُّعَاةِ إِلَی طَاعَتِکَ وَ الْقَادَةِ إِلَی سَبِیلِکَ وَ تَرْزُقُنَا بِهَا کَرَامَةَ الدُّنْیَا وَ الْآخِرَةِ . اللَّهُمَّ إِنَّا نَرْغَبُ إِلَیْکَ فِی دَوْلَةٍ کَرِیمَةٍ تُعِزُّ بِهَا الْإِسْلامَ وَ أَهْلَهُ وَ تُذِلُّ بِهَا النِّفَاقَ وَ أَهْلَهُ وَ تَجْعَلُنَا فِیهَا مِنَ الدُّعَاةِ إِلَی طَاعَتِکَ وَ الْقَادَةِ إِلَی سَبِیلِکَ وَ تَرْزُقُنَا بِهَا کَرَامَةَ الدُّنْیَا وَ الْآخِرَةِ . اللَّهُمَّ إِنَّا نَرْغَبُ إِلَیْکَ فِی دَوْلَةٍ کَرِیمَةٍ تُعِزُّ بِهَا الْإِسْلامَ وَ أَهْلَهُ وَ تُذِلُّ بِهَا النِّفَاقَ وَ أَهْلَهُ وَ تَجْعَلُنَا فِیهَا مِنَ الدُّعَاةِ إِلَی طَاعَتِکَ وَ الْقَادَةِ إِلَی سَبِیلِکَ وَ تَرْزُقُنَا بِهَا کَرَامَةَ الدُّنْیَا وَ الْآخِرَةِ .
Hossein Nouri Hamedani.
Qom Al-Muqaddasa - Seminari (Hawza) ya Kielimu.
14 Ramadhani 1446 inayosadifiana na 16 Machi 2025.
Your Comment