Ripoti ya shirika la habari la Ahlul Bayt(as)-ABNA- Dr. Abdullah Abdulhamid mmoja kati ya makhatibu wa Sala ya Ijumaa Misri katika hotuba yake ya Ijumaa katika Masjid Al-Mustafa alisema: Ukweli ni kwamba waalimu zetu wajitenga mbali sana na vyombo vya habari kutokana na sheria ya Kiislam na Qurani, Na kila asokua Muislam hasa Wakristo wa Misri lazima wajiunge na Uislam kama hawakufanya hivyo waadhibiwe.
Akiendelea kusema: Baadhi ya makhatibu wa kufuru wa Kiislam wasema kua Waislam na Wakristo ni wamoja na umoja wao umeshamili baina yao, Na Waislam hao walazimika kutowa mkono wa Idi inapofikia mwaka mpya wa Wakristo.
Dr. Abdullah Abdulhamid: Waislam watambue kua uadui wetu na hao umetajwa katika Qurani (na umekwisha dhihiri uadui na chuki baina yetu na nyinyi mpaka mtakapo muamini Mwenyezi Mungu peke yake.Qurani 60/4) Na sisi hatutofanya chochote kile dhidi yao ushahidi ni mapinduzi January ya Misri hatukuvunja Makanisa yao.
Aidha alisisitiza kwa kusema: Mtukufu Mtume(saw) alituma mawakili wake Najran kuwataka Nasara (Wakristo ) kukubali Uislam au kutowa kodi na kuwapa onyo kua wakipinga italazimika kupigana vita, Ama Masheikh kufuru wadai na kudhani wao ni Waislam walingania watu umoja baina ya Waislam na Wakristo ukizingatia maneno yao ni batili na hayana msingi wowote ule, Dini Tukufu ya Kiislam haikubaliani na Maneno hayo kwa kua Wakristo ni maadui wa Uislam hadi siku ya kiyama!!.
Hayo ni Madai ya ajabu ya Sheikh wa Kiwahabi huyo kunako ndugu zake wa Misri wasokua Waislam, Ila kakubali rasmi utawala haramu wa Israel ambao unaouwa ndugu zake Waislam na Qurani imeeleza wazi kua Mayahudi ndio maadui wa Uislam, Serikali ya Misri hadi sasa haijaongea kunako maneno makali ya Sheikh huyo wa Kisalafi.