Profesa wa Oxrord aleta jambo geni katika jamii kwa kufungua msikiti wapekee, anaouita kuwa ni msikiti usio na ubaguzi.
katika msikiti huu anaruhusu wanawake kuongoza Ibada na pia anaruhusu kuchanganyikana watu wa jinsia moja, vitu ambavyo vinapingwa vikali na nikinyume na utaratibu wa dini tukufu ya kiislamu.
Bwana Hargey, ambaye ni profesa katika chuo cha mafunzo ya kiisilamu mjini Oxford, Uingereza, ameufungua msikiti huu katika mji wa Cape town Afrika kusini.
Haegey alisema:"miaka 20 iliyopita, Afrika Kusini ilishuhudia mageuzi yaliyofanywa kwa njia ya amani. Kutoka katika enzi ya ubaguzi wa rangi hadi kwa demokrasia na tunahitaji kuwa na hali kama hiyo katika dini, ''
Hargey anadi kuwa, Lengo lake kufanya hivyo anasema ni kumkomboa mwanamke katika dini ya kiisilamu ambaye anasema ameachwa nyuma sana.Imekuwa ni ada kwa watu wanaotafuta umaarufu wa gafla kwenda kinyume na jamii, na hivi ndivyo tunavyoona kwa Hargey.
19 Septemba 2014 - 19:26
News ID: 638760
_541c82471afb5.jpg)
Profesa wa Oxrord aleta jambo geni katika jamii kwa kufungua msikiti wapekee, anaouita kuwa ni msikiti usio na ubaguzi.