19 Januari 2015 - 21:14
News ID: 665840

Haya ni mazishi ya Shahid Jihad Ammad Mughiyah ambaye amefariki kufuatia shambulizi lililofanywa na Israel dhidi ya wanajeshi wa Hizbollah na kuua askari 7, ambapo askari sita ni wa makomando wa Hizbullah na mmoja ni Jenerali wa jeshi la Jamhuri ya kiislamu ya Iran Jeneral Muhammad Ali Alahh Dodii. Shahid Jihad Ammad Mughiyah amezikwa katika makaburi ya Raudhatu Shahiidin, amezikwa pembeni ya kaburi la babake Shahiid Alhaj Ammad Mughniyah ambaye alikuwa ni Jeneral wa Jeshi la Hizbullah.