11 Desemba 2019 - 09:18
Jeshi la Somalia lazima shambulizi la al Shabab dhidi ya Ikulu ya Rais mjini Mogadishu

Jeshi la Somalia limetangaza kuwa, limewaangamiza wapiganaji 5 wa kundi la kigaidi la al Shabab waliojaribu kuingia na kuhujumu Ikulu ya Rais na hoteli moja iliyoko karibu na eneo hilo mjini Mogadishu.

(ABNA24.com) Vyombo vya usalama vya Somalia vimesema kuwa, askari usalama wa nchi hiyo wameua magaidi watatu katika lango kuu la kuingia Ikulu ya Rais na magaidi wengine wawili karibu na hoteli inayotumiwa sana na maafisa wa serikali na matajiri baada ya ufyatulianaji wa risasi ulioendelea kwa muda wa masaa mawili.  

Ripoti zinasema maafisa wa serikali waliokuwa katika hoteli hiyo walihamishiwa sehemu nyingine wakati wa majibizano hayo ya risasi.

Idhaa ya Andalusia inayotumiwa na wanamgambo wa al Shabab iimetangza kuwa, kundi hilo ndilo lililohusika na hujuma dhidi ya Ikulu ya Rais wa Somalia. Hujuma hiyo imetajwa kuwa ni ya aina yake katika kipindi cha miezi miezi ya hivi karibuni.

Duru za habari zinasema watu wasiopungua sita wamejeruhiwa katika hujuma hiyo wakiwemo wabunge wawili wa Somalia. 

..........
340