-
Habari Pichani | Darsa la Subhi ya Kiroho | Jamiat Al-Mustafa (S), Dar - Es- Salam - Tanzania
Shirika la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) - ABNA - Darsa la Akhlaq na Maadili ya Kiislamu linaendelea kila siku asubuhi katika Chuo cha Jamiat al-Mustafa (s) - Dar-es-Salam likibeba anuani ya Subhi ya Kimaanawi / Kiroho. Mwanadamu anatakiwa daima kuishi maisha ya kiroho. Maisha hayo ya kiroho, ndio maisha bora na yaliyojaa kuridhika na ukaribu kwa Mfalme Mwenye Uwezo, Mola wa Walimwengu wote.
-
Picha | Hafla kubwa ya Qur'an Tukufu kufanyika Jijini Dar-es-Salam, Chini ya Uongozi na Usimamizi wa Jamiat Al-Mustafa (s) Dar-es-Salam- Tanzania
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) - ABNA - Hojjatul Islam wal Muslimin, Dr. Ali Taqavi, Mwakilishi wa Jamiat Al-Mustafa (s) Dar-es-Salam - Tanzania kwa kushirikiana na Mwenyekiti wa JMAT-TAIFA, Samahat Sheikh Dr. Alhad Musa Salum, anaendelea na vikao mbalimbali na muhimu katika muktadha wa maandalizi ya Hafla kubwa ya Qur'an Tukufu itakayofanyika katika Uwanja wa Michezo wa Mkapa Jijini Dar-es- Salam. Hafla hii ya Qur'an Tukufu itawahusisha wasomaji mahiri wa Qur'an Tukufu kutoka Tanzania, Zanzibar na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Qur'an Tukufu ni Uhai wa Nyoyo.
-
Dua ya Kumail Bin Ziayad ikisomwa katika Madrasa ya Imam Ali (a.s) Zanzibar
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) - ABNA - Katika picha ni wanafunzi wa Hawzat Imam Ali (a.s) wakisoma Dua muhimu ya Kumail bin Ziyad ambayo husomwa kila Alkhamis Usiku wa Kuamkia Ijumaa. Dua hii ni muhimu na Muislamu unasisitizwa kuisoma kila wiki, ukishindwa usiache kuisoma kila Mwezi walau mara moja, na ukishindwa kabisa basi kwa Mwaka mara moja hakikisha unaisoma.
-
Habari Pichani | "Uhusiano kati ya Iran na Saudi Arabia utakuwa wa manufaa kwa nchi zote mbili /Kupanua uhusiano kati ya nchi hizi mbili kuna maadui"
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul Bayt (a.s) - ABNA -, Bwana Khalid bin Salman, Waziri wa Ulinzi wa Saudi Arabia amewasilisha ujumbe wa Mfalme wa nchi hii kwa Ayatollah Khamenei alasiri ya leo wakati wa kikao na Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu. Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza katika kikao hiki: "Tunaamini kuwa uhusiano kati ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Saudi Arabia utakuwa wa manufaa kwa nchi zote mbili na nchi hizo mbili zinaweza kukamilishana." Akisisitiza kwamba kupanuka kwa uhusiano kati ya nchi hizo mbili kuna maadui, Ayatollah Khamenei alibainisha: "Nia hizi za uhasama lazima zishindwe, na tuko tayari kwa hili."
-
Kiongozi wa Mapinduzi: Uhusiano kati ya Iran na Saudi Arabia utakuwa wa manufaa kwa nchi zote mbili / Kupanua uhusiano kati ya nchi hizi 2 kuna maadui
Katika kikao hicho Ayatollah Khamenei akiashiria baadhi ya maendeleo ya Iran amesema: Jamhuri ya Kiislamu iko tayari kuisaidia Saudi Arabia katika maeneo hayo.
-
Uhusiano wa Iran na Urusi | Waziri wa Mambo ya nje ya Iran apokelewa na Putin Jijini Moscow
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) - ABNA - Uhusiano wa Kidiplomasia baina ya Tehran na Moscow unazidi kuimarika zaidi na ni uhusiano usioweza kuvunjika, ni uhusiano wa muda mrefu kihistoria. Katika video hii fupi, Rais wa Urusi Vladmir Putin amempokea leo hii Waziri wa Mambo ya wa Iran, Mh. Sayyid Abbas Araqchi katika Ikulu ya Urusi, Jijini Moscow.
-
Habari Pichani | Darul - Qur'an yafunguliwa Jijini Mwanza kwa Jina la Imam Zainul - A'bidina (a.s)
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) - ABNA - Tarehe 20 - 04 - 2025, kwa mara ya kwanza itafunguliwa Darul - Qur'an Jijini Mwanza - Tanzania kwa Jina la Imam Zainul - A'bidina (a.s). Sherehe ya ufunguzi wa Shule hiyo ya Qur'an Tukufu itafanyika katika viwanja vya shule hiyo inayopatikana katika katika maeneo ya ILOGANZALA, Mtaa wa Saba Saba. Hafla ya ufunguzi itaanza muda wa saa saba na nusu / 7:30 baada Sala ya Adhuhuri. Wageni mbalimbali wa Taasisi Mbalimbali za Kiislamu wamealikwa katika hafla hiyo, wakiwemo: Viongozi wa Serikali, Baraza Kuu la Waislamu Tanzania, na Bilal Muslim Mission of Tanzania.
-
Al_Itrah Foundation Dar-es-salaam yatoa zawadi ya Qur'an ya Tarjama ya Kiswahili kwa Sheikh Walid Alhad Omar Kawambia, Sheikh wa Mkoa wa Dar-es-salaam
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) - ABNA - Leo hii, 17 April 2025, Al Itrah Foundation , Dar-es-salaam - Tanzania imefanya tukio la heshima lililofanyika kupitia Ofisi za Taasisi hii Jijini Dar-es-salaam, ikiwakilishwa na Bw. Khomeini Ruhullah, ambapo ilimkabidhi Sheikh wa Mkoa wa Dar-es-salaam - Sheikh Walid Alhad Omar Kawambia Qur'an Tukufu yenye Tafsiri ya Kiswahili kwa Kalamu ya Marhumu Sheikh Hassan Ally Mwalupa. Zawadi hii muhimu inatambua uzito wa maarifa, mshikamano wa Kiislamu na kiroho.
-
Maandalizi ya Hafla kubwa ya Qur'an Tukufu itakayojumuisha timu mbalimbali za Wasomaji wa Qur'an wa Tanzania, Zanzibar na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul- Bayt (a.s) - ABNA - Dr. Ali Taqavi, Rais wa Jamiat Al-Mustafa (s) yupo katika harakati muhimu za kuandaa Hafla kubwa ya Qur'an Tukufu itakayofanyika nchini Tanzania ikijumuisha Tanzania bara na Zanzibar. Katika picha hizi ni tukio za kukagua na kutembelea uwanja mkubwa wa michezo Jijini Dar-es-Salam - Tanzania, ambao utatumika kwa ajili ya hafla kubwa ya Qur'an Tukufu itakayohudhuriwa na timu kubwa ya wasomaji mahiri wa Qur'an Tukufu kutoka katika nchi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
-
Kipindi cha Nasaha za Ulimwengu | Kwa nini Mwanadamu anafanya Kiburi wakati asili yake ni Maji Machafu?!
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) - ABNA - IBN TV AFRIKA imeendesha na inaendeleza kipindi chake muhimu cha Nasaha za Ulimwengu. Kupitia Kipindi hiki cha "Nasaha za Ulimwengu" Sheikh Ramadhan Masemo ametoa nasaha muhimu kwa Wanadamu na Walimwengu kwa ujumla ambapo ametanguliza swali hili muhimu: Ni kwa nini Mwanadamu anafanya Kiburi wakati asili yake ni Maji Machafu?! Hutamani hata kiyatazama? Sasa kiburi cha nini?!. Kisha akasisitiza katika kunukuu maneno hayo ya Imam Ali (a.s) aliposema: "Mwanadamu unajivunia nini wakati asili yako ni maji machafu? Halafu wewe kama Mwanadamu unatembea na uchafu tumboni?! Na baada ya kufa kwako unageuka na kuwa mzoga unaotoa harufu mbaya sana!" . Sasa kwa nini ujigambe kwa mali, kwa kipaji ulichopewa, uwe na kiburi?. Yote hayo ni mambo yanayopita na tutayaacha hapa hapa duniani.
-
Habari Pichani | Harakati za Kielimu na Kitamaduni Katika Hawza ya Zainul - A'bidina (a.s) - Burundi + Audio
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlu-Bayt (a.s) - ABNA - Hawza ya Imam Zainul - A"bidina (a.s) nchini Burundi inaendelea na harakati zake za Kielimu na Utamaduni wa Kiislamu. Katika picha ni moja ya Harakati za Kielimu na Kitamaduni zinazoendelea kila siku katika Hawza ya Zainul - A'bidina (a.s) - iliyopo Burundi ambapo kila siku Wanafunzi hujipanga katika mistari na kusoma Dua mbalimbali za kila siku, katika picha ni tukio la kusoma Dua ya Siku ya Alkhamisi (kama inavyoonekana hapo chini katika Maandidhi na Audio kwa sauti ya Aba Dhar Al-Halawaji).