-
Kansela mpya wa Ujerumani aionya Marekani iache kuingilia siasa za ndani
Kansela mpya wa Ujerumani, Friedrich Merz, leo Jumatano ameionya Marekani dhidi ya kuingilia siasa za ndani za nchi yake.
-
Guterres ataka India na Pakistan zisitishe operesheni za kijeshi
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, ameelezea wasiwasi wake kuhusu operesheni za kijeshi zinazofanywa na jeshi la India kwenye mstari wa usimamizi na mpaka wake wa kimataifa na Pakistan.
-
Vyombo vya usalama vya Israel vyaonya kuhusu kupanua vita Ukanda wa Gaza
Vyombo vya usalama vya utawala wa Kizayuni wa Israel vimewatahadharisha viongozi wa utawala huo kwamba kupanuliwa oparsheni za kijeshi katika Ukanda wa Gaza kutapelekea kuuawa mateka wa Kizayuni wanaoshikkiliwa na wanamapambano wa Kipalestina.
-
Ansarullah: Mapatano na Marekani hayatazuia mashambulizi ya Yemen dhidi ya Israel
Harakati ya Muqawama ya Ansarullah ya Yemen imesema kuwa kusitishwa kwa mashambulizi ya anga ya Marekani dhidi ya Yemen mkabala wa kusitisha mashambulizi dhidi ya meli za kivita za Marekani katika Bahari ya Shamu hakutabadilisha msimamo wa Yemen kuhusu kushambulia Israel.
-
Russia na Iran zasisitiza kushirikiana zaidi katika siasa za kigeni
Marais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Russia wamesisitiza juu ya azma ya nchi zao ya kushirikiana zaidi katika uga wa siasa za kigeni.
-
Jibu la mkato la Iran kwa porojo la Netanyahu
Amir-Saeid Iravani, Balozi na Mwakilishi wa kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa ameliandikia barua Baraza la Usalama la umoja huo kujibu porojo na upayukaji wa waziri mkuu wa utawala wa Kizayuni Benjamin Netanyahu dhidi ya Iran.
-
Maonyesho ya 36 ya Kimataifa ya Vitabu ya Tehran yafunguliwa
Maonyesho ya 36 ya Kimataifa ya Vitabu ya Tehran yamefunguliwa leo asubuhi katika sherehe iliyohudhuriwa na viongozi wa ngazi za juu wakiwemo Waziri wa Utamaduni na Muongozo wa Kiislamu, Abbas Salehi, na Spika wa Bunge la Iran, Mohammad Bagher Ghalibaf.
-
Russia yaituhumu Ulaya na NATO kuwa zinajiandaa kwa makabiliano ya moja kwa moja ya kijeshi
Katibu wa Baraza la Usalama la Russia, Sergei Shoigu, amelituhumu shirika la kijeshi la nchi za Magharibi, NATO na Umoja wa Ulaya kuwa zinaandaa mzozo wa moja kwa moja wa kijeshi na Moscow.
-
Imam Khamenei: Ustaarabu wa Kiislamu ni kinyume cha ustaarabu wa sasa wa kimaada
Katika ujumbe wake kwa kongamano la "Miaka 100 wa Kuanzishwa Hauza ya Qum nchini Iran," Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa: "Kazi muhimu zaidi ya Hauza na taasisi ya kielimu ya vyuo vikuu vya kidini, ni kufikisha ujumbe wa wazi na kuweka msingi wa ustaarabu mpya wa Kiislamu."
-
Dkt. Ali Taqavi, Mwakilishi wa Jamiat Al-Mustafa (s) Dar es Salaam – TanzaniaAfanya Ziara ya Mshikamano na Wanazuoni wa BAKWATA Mkoani Tanga + Picha
Ziara hii ni muendelezo wa juhudi za kuimarisha mawasiliano kati ya Madhehebu mbalimbali za Kiislamu na kujenga jukwaa la pamoja la kuhudumia jamii ya Kiislamu nchini Tanzania.
-
Bangladesh | Mkutano wa wageni wa Kimataifa katika kumbukumbu ya miaka 100 ya kuanzishwa upya kwa Hawza ya Elimu ya Qom na Mwakilishi wa Syed Khamenei
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa Shirika la Habari la Ahlul Bayt (AS) - ABNA, wageni wa kimataifa wa kongamano la maadhimisho ya miaka mia moja ya kuanzishwa upya kwa Hawza ya Elimu ya Qom walikutana na Mwakilishi wa Ofisi ya Kiongozi wa Mapinduzi katika nchi ya Bangladesh.
-
"Video | Hatuwezi kuangalia miili dhaifu ya Watoto wa Gaza na tukabaki kimya"
Shirika la Habari la Kimaitaifa la Ahlul-Bayt (a.s) - ABNA - Muhammad al-Bukheiti, Mjumbe wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Ansarullah ya Yemen: "Tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutupatia neema ya kutekeleza jukumu letu mbele ya watu wa Gaza. Kukatwa katwa vipande miili yetu ni bora zaidi kwetu kuliko kuwa na mioyo migumu kama mawe."
-
Ujumbe wa Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi kwa mkutano wa kumbukumbu ya miaka mia moja (100) ya kuanzishwa upya kwa Chuo cha Dini cha Qom:
Ayatollah Khamenei: Jukumu la (Hawza) Chuo cha Kidini ni Kuchora Mipaka Mikuu na Midogo ya Ustaarabu mpya wa Kiislamu
"Kazi kuu na ya msingi ya Hawza ni (البَلاغُ المُبین) kufikisha ujumbe wa dini kwa uwazi na ufasaha (ubalighi wa wazi - Kwa maana: Kufikisha ujumbe kwa uwazi na uthabiti na kwa namna ambayo haiachi shaka yoyote -). Miongoni mwa vielelezo vyake muhimu kabisa ni kuchora na kueleza kwa uwazi mistari (mipaka) mikuu na ya kando ( au midogo) ya ustaarabu mpya wa Kiislamu, pamoja na kuifafanua, kuieneza, na kuikuza katika jamii kama sehemu ya utamaduni."