Sisitizo hilo limetolewa katika mazungumzo ya simu ya Rais wa Iran Masoud Pezeshkian na mwenzake wa Russia Vladmir Putin.
Russia na Iran, ambazo kwa mtawalia zimeshuhudia vikwazo vya kidhalimu zaidi vya Magharibi dhidi yao, zilitiliana saini Mkataba wa Ushirikiano wa Kimkakati Kamili kati mnamo Januari 17, 2025. Rais wa Iran Masoud Pezeshkian na Rais wa Russia Vladimir Putin walitia saini makubaliano hayo ya kina na kusisitiza haja ya kutekeleza vipengee vyake.
Marais wa Russia na Iran Vladimir Putin na Masoud Pezeshkian wamekubaliana kuongeza ushirikiano wa pamoja ili kuimarisha uratibu katika sera za kigeni, ikulu ya Kremlin ilisema katika taarifa Jumanne.
Maraiis hao wamesisitiza pia upanuzi wa mahusiano ya biashara na uwekezaji yenye manufaa kwa pande zote mbili, ikiwa ni pamoja na kupitia utekelezaji wa miradi mikubwa ya pamoja katika nyanja za usafirishaji na nishati.
Sisitizo la Putin na Pezeshkian kuhusu ushirikiano wa kiuchumi na miradi ya pamoja katika uga wa usafirishaji na nishati inadhihirisha azma ya Russia na Iran ya kutumia uwezo uliopo na kuimarisha uhusiano wa kibiashara.
Aidha katika mazungumzo hayo ya simu, Rais Putin alitoa mkono wa pole kwa Rais Pezeshkian na taifa la Iran kufuatia mlipuko wa hivi karibuni katika Bandari ya Shahid Rajaei ambapo makumi ya watu walipoteza maisha yao.
342/
Your Comment