23 Julai 2025 - 15:04
Rais wa Tunisia Amkabili Mshauri wa Trump kwa Picha za Watoto wa Gaza Wanaokaribia Kufa kwa Njaa, huku wakiwa udondo ili wabakie hai + Video Fupi

Rais wa Tunisia Qais Saeed, katika mkutano rasmi na Masaad Boulos – mshauri mwandamizi wa Donald Trump kwa masuala ya Mashariki ya Kati na Afrika – amemkabili hadharani kwa kuonesha picha za kusikitisha za watoto wa Gaza wanaoteseka kwa njaa, wakilazimika kula udongo kutokana na ukosefu wa chakula.

 Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Rais wa Tunisia Qais Saeed, amemkabili kisawa sawa mshauri mwandamizi wa Donald Trump (Masaad Boulos) katika masuala ya Mashariki ya Kati na Afrika - ambapo amemuonesha picha za kusikitisha za watoto wa Gaza wanaoteseka kwa njaa, huku wakilazimika kula udongo kutokana na ukosefu wa chakula angalau wabakie hai katika siku kadhaa huenda huruma ya Mwenyezi Mungu ikashuka juu yao kwa kuwaokoa na maadui wa binadamu (wazayuni).

Maelezo Muhimu ya Tukio Hilo:

1- Tukio hilo limefanyika katika Ikulu ya Qasr al-Qartaj, Tunisia.

2- Mgeni: Masaad Boulos, Mshauri wa Trump.
3- Kitendo cha Rais: Kuonesha picha za watoto wa Palestina waliodhoofika kwa njaa, wakilia na kula udongo kimeleta hisia kubwa ya huruma kwa watu wote huru duniani na walio na utu na ubinadamu.
4- Kauli Kali ya Rais Qais Saeed:

“Nadhani picha hizi ni maarufu. Mtoto huyu analia kwenye ardhi iliyokaliwa kwa mabavu – hana chakula chochote, amebeba udongo tu… Na huyu mwingine yuko karibu kufa kwa njaa. Hii siyo halali, wala haikubaliki kibinadamu!”

Kauli Zenye Uzito kutoka kwa Rais Saeed:

Kuhusu uhalali wa jamii ya kimataifa:

“Je, huu ndio uhalali wa kimataifa unaosemwa kila siku? Kila saa watu wa Palestina wanapitia maafa haya – huu ni udhalilishaji wa dhamira ya ubinadamu.”

Rais wa Tunisia Amkabili Mshauri wa Trump kwa Picha za Watoto wa Gaza Wanaokaribia Kufa kwa Njaa, huku wakiwa udondo ili wabakie hai + Video Fupi

Wito wa kuchukua hatua:

“Wakati umefika kwa ubinadamu kuamka – lazima jamii ya kibinadamu isimame dhidi ya uhalifu huu unaofanywa dhidi ya watu wa Palestina.”

Kwa mataifa ya Kiarabu:

“Masuala ya mataifa ya Kiarabu yanapaswa kutatuliwa na watu wa mataifa hayo wenyewe, bila uingiliaji kutoka nje.”

Masuala Mengine Yaliyojadiliwa:

1- Janga la Gaza na jinai za Israel.

2- Tatizo la ugaidi katika kanda ya Kiarabu.

3- Msimamo wa Tunisia kuhusu kutoingiliwa kwa nchi nyingine.

4- Maendeleo ya ushirikiano wa kimkakati kati ya Tunisia na mataifa rafiki.

Mwisho:
Rais Qais Saeed ametoa ujumbe mzito kwa ulimwengu - kwamba heshima ya jamii ya kimataifa iko shakani mbele ya watoto wanaokufa kwa njaa Gaza. Kitendo chake cha kuonesha picha hizo mbele ya mjumbe wa Marekani kinaonesha msimamo wa dhati wa Tunisia dhidi ya uhalifu wa kivita unaofanywa na utawala wa Kizayuni kwa msaada wa nchi za Magharibi.

Wito kwa Mataifa Huru: Kuamka, kulaani wazi jinai za Israel, na kuchukua hatua thabiti kwa ajili ya kulinda haki za watu wa Palestina.

Your Comment

You are replying to: .
captcha