21 Julai 2025 - 20:38
Katika Kuadhimisha Walima ya Mwanae, Sheikh Dkt. Alhad Mussa Salum Ahuisha kwa Vitendo Hadithi ya Mtume (s.a.w.w) ya Kukirimu Wageni +Klipu Fupi

Mtume (s.a.w.w) alisema: "Mwenye kumuamini Allah na Siku ya Mwisho basi amkirimu mgeni wake." (Sahih al-Bukhari na Sahih Muslim).

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Klipu hii fupi inaonyesha namna Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT-TAIFA) - Sheikh Dkt.Alhad Mussa Salum alivyoongoza njia katika kuwakirimu vyema wageni wake waliohudhuria katika "Walima ya Mwanae Islah", iliyofanyika kwa mafanikio makubwa katika Ukumbi wa DYCC Temeke.

Katika Kuadhimisha Walima ya Mwanae, Sheikh Dkt. Alhad Mussa Salum Ahuisha kwa Vitendo Hadithi ya Mtume (s.a.w.w) ya Kukirimu Wageni +Klipu Fupi

Samahat Sheikh Dkt.Alhad Mussa Salum ameitekeleza vyema Hadithi maarufu ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) kuhusu kukirimu mgeni - (wageni kwa kuwakirimu vyema wageni wake) - iliyopokelewa na wengi miongoni mwa Wanahadithi. Mtume (s.a.w.w) alisema:

"Mwenye kumuamini Allah na Siku ya Mwisho basi amkirimu mgeni wake." (Sahih al-Bukhari na Sahih Muslim).

Katika Kuadhimisha Walima ya Mwanae, Sheikh Dkt. Alhad Mussa Salum Ahuisha kwa Vitendo Hadithi ya Mtume (s.a.w.w) ya Kukirimu Wageni +Klipu Fupi

Samahat Sheikh Dkt. Alhad Mussa Salum, mbali na kuwa katika Hafla ya "Walima wa Mwanae" katika kufurahia jambo tukufu la Ndoa, ameitumia fursa hiyo kuonyesha kwa vitendo namna inavyotakiwa kwa Muislamu kuyafanyia kazi kwa vitendo maelekezo ya Mtume Muhammad (saww) kuhusiana na Ukarimu kwa Wageni.

Kwa hakika moja ya alama za imani ya kweli kwa Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho, ni tabia ya ukarimu kwa wageni.

Mtume (s.a.w.w) alihimiza sana kuwaheshimu na kuwahudumia wageni, kwa kuwa hilo ni miongoni mwa maadili mema yanayojenga jamii yenye huruma na mshikamano.

Katika Kuadhimisha Walima ya Mwanae, Sheikh Dkt. Alhad Mussa Salum Ahuisha kwa Vitendo Hadithi ya Mtume (s.a.w.w) ya Kukirimu Wageni +Klipu Fupi

Katika riwaya nyingine, Mtume (s.a.w.w) alisema:

"Mgeni ana haki ya kukaribishwa kwa siku tatu, na zawadi bora zaidi kwa mgeni ni ya siku moja. Ikiwa atakaa zaidi ya hapo, basi ni sadaka kwake." (Sahih al-Bukhari na Muslim).

Your Comment

You are replying to: .
captcha