7 Mei 2025 - 21:40
Source: Parstoday
Jibu la mkato la Iran kwa porojo la Netanyahu

Amir-Saeid Iravani, Balozi na Mwakilishi wa kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa ameliandikia barua Baraza la Usalama la umoja huo kujibu porojo na upayukaji wa waziri mkuu wa utawala wa Kizayuni Benjamin Netanyahu dhidi ya Iran.

Katika barua yake hiyo kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Iravani amesema: "chokochoko zozote za kijeshi zitakazofanywa na Marekani au wakala wake -utawala wa Kizayuni-, iwe ni hatua itakayochukuliwa dhidi ya mamlaka ya kujitawala, umoja wa ardhi yote, au maslahi muhimu na ya kitaifa ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, zitakabiliwa na jibu la haraka, mwafaka na lenye uhalali wa kisheria".

Jibu la mkato la Iran kwa porojo la Netanyahu

Barua ya Balozi wa Iran katika Umoja wa Mataifa imebainisha kuwa, hatua zinazochukuliwa na taifa la Yemen zinatokana na maamuzi huru yanayotekelezwa kwa msingi wa taifa hilo kutumia haki yake ya kujitawala ya kupinga uvamizi na uchokozi dhidi ya mamlaka yake ya kujitawala na umoja wa ardhi yake yote; na zimechukuliwa pia kuonyesha mshikamano na watu wa Palestina ambao wanaandamwa na mashambulizi ya mtawalia na yasiyokubalika kisheria.

Barua hiyo imeendelea kueleza kuwa, jaribio lolote la kuhusisha hatua hizo halali na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni upotoshaji wa makusudi wa ukweli halisi wa mambo na ni hatua ya kutapatapa ya kujaribu kuibabaisha jamii ya kimataifa iache kuzingatia chimbuko halisi la mgogoro unaoendelea hivi sasa katika eneo, ambalo ni: jinai kubwa, za wazi kabisa na za matawalia zinazofanywa na utawala wa Kizayuni huko Ghaza na Ukingo wa Magharibi yakiwemo mauaji ya kimbari, uhalifu wa kivita na jinai dhidi ya binadamu pamoja na uchokozi na hujuma zisizo na kikomo za Marekani dhidi ya Yemen.

Iravani amebainisha katika barua yake hiyo kuwa, matamshi ya aina hiyo ya kuchochea vita na kuzusha mivutano, ambayo yamechanganyika waziwazi na vitisho vya kutumia nguvu dhidi ya nchi inayojitawala na mwanachama wa Umoja wa Mataifa, ni ukiukaji mkubwa na wa wazi wa msingi mkuu wa sheria za kimataifa na Hati ya Umoja wa Mataifa.

Esmail Baghaei, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, naye pia amelaani vikali mashambulio ya kijeshi yaliyofanywa na utawala wa Kizayuni dhidi ya bandari ya Al Hudaydah na miundombinu mingine ya Yemen na kuyaelezea kuwa ni jinai ya wazi na ukiukaji mkubwa wa misingi na kanuni za sheria za kimataifa.

Huku akiashiria ukweli kwamba mashambulizi ya utawala wa Kizayuni dhidi ya bandari, majengo ya viwanda na makazi ya raia nchini Yemen yanafanywa kwa ushiriki na uungaji mkono wa Marekani, Baqhaei amesema, hujuma hizo ni uvunjaji wa waziwazi wa sheria na ukiukaji wa kanuni na misingi ya Hati ya Umoja wa Mataifa kuhusiana na kuheshimu mamlaka ya kitaifa na umoja wa ardhi yote ya nchi; na akataka jamii ya kimataifa na nchi za eneo zichukue hatua madhubuti na athirifu kusimamisha mwenendo huo wa mauaji na uharibifu unaofanywa na Marekani na utawala wa Kizayuni katika nchi za Kiislamu.

Jibu la mkato la Iran kwa porojo la Netanyahu

Katika siku za hivi karibuni, kwa mara nyingine tena Netanyahu amerudia kutoa tuhuma zake zisizo na msingi na kuzihusisha kiupotoshaji na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran hatua za taifa la Yemen za kujibu mapigo kwa jinai zinazofanywa katika Palestina inayokaliwa kwa mabavu.

Waziri mkuu wa utawala wa Kizayuni ametoa vitisho vya waziwazi dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran akidai kuwa Israel italipiza kisasi, si kwa Yemen pekee, bali dhidi ya Iran pia. Waziri wa ulinzi wa Marekani Pete Hegseth naye pia ameunga mkono matamshi hayo ya upayukaji ya Netanyahu.

Misimamo ya Netanyahu dhidi ya Iran inaonyeshwa katika hali ambayo viongozi wa utawala wa Kizayuni wanafuatiliwa kisheria na mahakama za kimataifa kwa sababu ya mauaji ya kimbari na jinai zinazofanywa kwa kuratibiwa na jeshi la utawala huo ghasibu katika Ukanda wa Ghaza.

Mhimili wa uovu wa Kimarekani na Kizayuni umeelekeza propaganda zake katika kuchafua sura ya vikosi vya Muqawama katika eneo katika hali ambayo, maoni ya umma katika Ulimwengu wa Kiislamu yamedhihirisha waziwazi kuchukizwa na jinai za Wazayuni kwa kushiriki katika maandamano makubwa katika miezi ya hivi karibuni.

Makundi ya Muqawama katika eneo yakiwemo ya Palestina, Lebanon na Yemen hayahitaji uungaji mkono wa serikali zozote na yanatumia uwezo wao wenyewe kukabiliana na Marekani na utawala wa Kizayuni. Mijibizo ya kutapatapa ya utawala wa Kizayuni katika kukabiliana na Muqawama wa Yemen na Palestina inaonyesha kuwa Wazayuni na waungaji mkono wa Tel Aviv yaani Marekani hawana uwezo tena wa kukabiliana na Muqawama.

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imekuwa ikisisitiza kila mara kuhusu haki yake ya kulinda umoja wa ardhi yake yote na kutoa jibu mwafaka kwa vitisho na chokochoko zitakazoanzishwa na utawala wa Kizayuni na muungaji mkono wake mkuu, Marekani katika eneo.

Uungaji mkono usio na kikomo wa Marekani na nchi za Magharibi kwa kikosi chao cha niaba na cha uwakala katika eneo, yaani utawala wa Kizayuni bado haujakoma; na kimsingi, ni mhimili wa Kimarekani na Kizayuni ndio unaopaswa kuwajibishwa kwa jinai zake za kinyama unazofanya huko Ghaza na Yemen.../

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha