7 Mei 2025 - 21:44
Source: Parstoday
Vyombo vya usalama vya Israel vyaonya kuhusu kupanua vita Ukanda wa Gaza

Vyombo vya usalama vya utawala wa Kizayuni wa Israel vimewatahadharisha viongozi wa utawala huo kwamba kupanuliwa oparsheni za kijeshi katika Ukanda wa Gaza kutapelekea kuuawa mateka wa Kizayuni wanaoshikkiliwa na wanamapambano wa Kipalestina.

Vyombo vya usalama vya Israel vimetoa indhari kwa viongozi wa kisiasa wa utawala huo kwamba kupanua oparesheni za kijeshi za nchi kavu katika Ukanda wa Gaza kwa mujibu wa uamuzi uliochukuliwa na baraza kisiasa na kiusalama la utawala huo kunayaweka hatarini maisha ya mateka wa utawala huo wanaoshikiliwa huko Gaza. 

Viongozi wa usalama wa utawala wa Israel pia wamesisitiza kuwa kuendelea oparesheni za kijeshi katika Ukanda wa Gaza kunapungua uwezekano wa kufikishwa chakula katika maeneo wanaposhikiliwa mateka hao wa Kizayuni jambo ambalo litapelekea mateka hao kubaki bila ya chakula na maji wakiwa mahandakini na kuaga dunia katika kipindi kifupi. 

wakati huo huo, jeshi la utawala wa Israel limeeleza wasiwasi wake kuhusu kuuawa mateka wa Kizayuni na kueleza kuwa katika mazingira hayo kuna uwezekano miili ya mateka hao pia isipatikane abadan.

Kabla ya hapo, Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) ilisisitiza kuwa kukubali serikali ya Israel kuendelea mashambulizi ya kijeshi katika Ukanda wa Gaza ni uamuzi wa kuwatoa kafara mateka wa Kizayuni wanaoshikiliwa huko Gaza. 

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha