-
Utabiri wa Mazuwwari 8 Milioni Katika Siku za Mwisho za Mwezi wa Safar
Naibu wa Kitengo cha Utamaduni, Jamii na Hija wa Mkoa wa Khorasan Razavi, Hojjatoleslam Ali Asgari, amesema kuwa idadi ya mazuwwari katika siku za mwisho za mwezi Safar imeongezeka kwa kiasi kikubwa ikilinganishwa na mwaka uliopita. Kwa kuzingatia likizo zinazokaribia, inatarajiwa kuwa idadi ya mazuwwari itafikia takriban milioni 8.
-
Kuongezeka kwa Idadi ya Mashahidi wa Njaa Gaza hadi 269
Wizara ya Afya ya Ukanda wa Gaza imetangaza kuwa katika saa 24 zilizopita watu wengine watatu wamepoteza maisha yao kutokana na njaa na ukosefu wa chakula.
-
Hamza(ra), Bendera ya Kwanza ya Uislamu
Hamza bin Abdulmuttalib (ra), ami yake Mtume wa Uislamu(saww), anajulikana kama Bendera ya kwanza ya Uislamu. Kwa ujasiri na kujitolea kwake katika kumtetea Mtume na mafundisho ya Kiislamu, alicheza nafasi muhimu katika kueneza Uislamu. Hamza hakuwa tu shujaa katika uwanja wa vita, bali pia alikuwa mfano na mlinzi wa Waislamu, daima akiwa upande wa Mtume na kwa msimamo wake, alitia nguvu na matumaini katika nyoyo za waumini.
-
Kwanini Idadi ya Mazuwari Karbala Inaongezeka?:
Ukarimu wa Iraq kwa Mazuwwari na Ukandamizaji wa Saudia kwa Mahujaji: Tofauti ya Idadi ya Mahujaji na Mazuwari
Uhuru wa Kiimani -Nchini Iraq, kila Muumini ana uhuru wa kutekeleza ibada zake kulingana na Dhehebu lake bila bughudha. Hali ni tofauti na Saudi Arabia ambapo Mahujaji wengine huadhibiwa wakituhumiwa kufanya vitendo vya “shirk” kwa mujibu wa mtizamo wao.
-
Mawaziri wa Mambo ya Nje wa China na Pakistan Wawasili Kabul, Afghanistan
Waziri wa Mambo ya Nje wa China alipokelewa na Amir Khan Muttaqi, Waziri wa Mambo ya Nje wa Serikali ya Kaimu ya Afghanistan, na kufanya naye mazungumzo. Wakati huo huo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Pakistan alipokelewa na Hanafi Wardak, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Serikali ya Taliban.
-
Ripoti ya Picha | Hafla ya Tatu ya Kitaifa ya Kuwatambua na Kuwapongeza Wafanyakazi na Wadau wa Misikiti Nchini +Picha
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) –ABNA– Mkutano wa Tatu wa Kitaifa wa Kuwatambua na Kuwapongeza Wahudumu na Waendeshaji wa Misikiti kote nchini, ukiwa na kauli mbiu ya “Kama Nusrullah”, umefanyika asubuhi ya leo Jumatano, tarehe 20 Agosti, 2025 katika ukumbi wa Shabistan ya Imam Ali (a.s) ndani ya Msikiti Mtukufu wa Jamkaran (Nchini Iran), kwa kuhudhuriwa na viongozi wa kitaifa na wa kijeshi.
-
Habari Pichani | Mdahalo wa Kitaifa ulioratibiwa na Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT) kwa kushirikiana na Global Peace Foundation
Akizungumza katika mdahalo huo, Sheikh Dkt. Al-Hadi Mussa Salum, Mwenyekiti wa JMAT, alisema: "Uchaguzi ni fursa ya kuonyesha uzalendo na kuchagua viongozi kwa njia ya amani".
-
JMAT TAIFA:
Mdahalo wa Viongozi wa Dini na Siasa: Wito wa Kudumisha Amani na Demokrasia Safi kuelekea Uchaguzi Mkuu
Sheikh Dkt. Al-Hadi Mussa Salum: "Amani na Utulivu nchini ni msingi wa maendeleo ya Taifa na Ustawi wa kila Mtanzania".