Main Title

source : ABNA
Jumamosi

18 Januari 2020

07:59:34
1003263

Ayatollah Khamenei (ra) katika kuelezea mazingira ya ushukaji wa aya hizo amesema kuwa ni aya zilizoshuka katika mji wa Maka, katika kipindi ambacho Waislamu walikuwa wapo katika mapambano mazito na harakati za ukafiri. “..Aya hizi zilishuka wakati wa mazingira magumu mno, lakini zilikuja kuwapa bishara njema Waislamu ya kwamba masiku ya Mwenyezi ni kwa ajili yenu, na kwa kushukuru kwenu basi ushindi mkubwa upo mbele yenu pia..” aliongezea Ayatollah Khamenei.

Kiongozi mkuu wa mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, Ayatollah Sayyed Khamenei katika sala ya Ijumaa ya kihistoria 17/1/2020 mjini Tehran, Iran  amesema kuwa matukio makuu mawili ambayo ni uhudhuriaji wa watu katika mazishi ya aliyekuwa kiongozi wa jeshi la mapinduzi, Qasem Soleimani pamoja na waambata wake, na tukio la majeshi ya mapinduzi kushambulia ngome za Kimarekani za Ainul Asad ni matukio yenye kuashiria uhakika wa siku za mwenyezi Mungu.

Aidha pia ameongezea kuwa uhudhuriaji wa wananchi katika matukio hayo ni ishara kubwa ya dhamira na nia yao katika kupambana na shetani mkubwa, na kwamba njia ya pekee ya kuweza kuendeleza jambo hili ni kujizatiti katika sekta mbalimbali.

Ayatollah Khamenei katika hotuba yake ya kwanza ya sala hiyo alianza kuwausia watu wote kunako kushikamana na kumcha Mungu, ambapo swala la ushindi, tawfiq ya Mwenyezi Mungu, utatuzi katika maswala binafsi na hata kijamii hupatikana katika kumcha Mungu. Na kisha akaanza mazungumzo yake ya asili kwa kutanguliza aya zinayopatikana katika Surat Ibrahim zenye kuzungumzia umuhimu wa masiku ya Mwenyezi Mungu pamoja na kuyatukuza na kumshukuru Mwenyezi Mungu juu ya masiku hayo.

Ayatollah Khamenei (ra) akizungumzia masiku ya Mwenyezi Mungu amesema kuwa amri ya Mwenyezi Mungu kwa Nabii Mussa kunako kuyakumbuka na kuyatukuza masiku ya Mwenyezi Mungu ni ishara tosha ya umuhimu wa masiku hayo na nafasi yake katika kuongoa watu wenye subira na shukrani, kama ambavyo ameashiria watu wenye subira ni wale ambao daima huwa na hali ya kusimama thabiti na wala si wenye kutolewa katika njia kwa vitu vidogovidogo, na wenye shukrani pia ni watu ambao baada ya kutambua neema za Mwenyezi Mungu zilizo wazi na hata zilizojificha hutambua thamani yake na kuhisi kwamba wana majukumu juu ya neema hizo walizopewa na Mwenyezi Mungu.

Ayatollah Khamenei (ra) katika kuelezea mazingira ya ushukaji wa aya hizo amesema kuwa ni aya zilizoshuka katika mji wa Maka, katika kipindi ambacho Waislamu walikuwa wapo katika mapambano mazito na harakati za ukafiri. “..Aya hizi zilishuka wakati wa  mazingira magumu mno, lakini zilikuja kuwapa bishara njema Waislamu ya kwamba masiku ya Mwenyezi ni kwa ajili yenu, na kwa kushukuru kwenu basi ushindi mkubwa upo mbele yenu pia..” aliongezea Ayatollah Khamenei.

Katika kuendelea na mazungumzo yake, Ayatollah Khamenei ameashiria kwamba wiki mbili zilizopita zilikuwa ni wiki za kipekee sana na zenye kuwa na matukio mengi mno mazuri na mabaya, lakini yote ni yenye kuacha mafunzo kwa taifa la Iran. Pia kwa kutumia anuani ya masiku ya Mwenyezi Mungu katika masiku haya ni kutokana na athari zake zisizo kifani ndani ya Iran na Iraq hasa katika kuwakirimu na kuwatukuza mashahidi. “..Siku ya Mwenyezi Mungu yaani ni siku ya kushuhudia nguvu za Mwenyezi Mungu katika utendaji, na kwa minajili hiyo kitendo cha mamilioni ya watu nchini Iran, Iraq na sehemu nyinginezo ulimwenguni kumiminika barabarani kutokana na kuuwawa kwa Qasem Soleimani na hatimaye kuonyesha mshikamano wa ulimwengu, pia ni katika masiku hayo, kwa sababu tu utukufu na ukubwa huu hauna chanzo tofauti na nguvu za Mwenyezi Mungu pekee..” alisema Ayatollah Khamenei.

Aidha pia Ayatollah Khamenei ameitaja siku ya makombora ya Jeshi la Sepah kushambulia kambi za Marekani kuwa i katika masiku ya Mwenyezi Mungu, kutokana na kwamba Taifa litokee kupata nguvu na kushambulia adui mwenye kiburi na movu, hii pia ni ishara ya uwezo wa nguvu ya Mwenyezi Mungu, hivyo siku hii kubwa pia ni katika masiku ya Mwenyezi Mungu.

Kiujumla kwa mujibu wa  Ayatollah Khamenei masiku ya Mwenyezi Mungu ni masiku yenye kuacha historia zenye kudumu katika maisha na hata kiroho pia, na katika kusifia mshikamano wa taifa la Iran amesema “..Kwa hakika taifa la Iran ni la watu wenye subira na kushukuru, kwa maana katika miaka yote wamekuwa wakisimama kwa uthabiti na shukrani za kuigwa kote...”.

Aidha katika kuelezea utukufu wa Mwenyezi Mungu katika tukio la kuagwa kwa Qasem Soleimani, Ayatollah Khamenei (ra) ameuliza swali kwa kusema “...Baada ya miaka 41 ya mapinduzi, je, kuna nguvu nyingine tofauti na ya Mwenyezi Mungu yenye uwezo wa kuleta muujiza na upendo wa umma kama huu?..”  akiashiria uwepo wa nguvu ya kimaana zaidi katika tukio hilo ambalo pia amelitaja ni alama ya kuashiria umoja wa watu katika kuungana mkono na Imamu aliye hai.

Pia akizungumzia tukio la kuuwawa Qasem Soleimani Ayatollah Khamenei amesema kuwa kulikuw ana jitihada za mataifa kama vile Israel na Marekani kutaka kumchafua Qasem Soleimani na kuwa alikuwa ni gaidi, lakini angalia namna ambavyo Mwenyezi Mungu ameweza kubadili malengo yao, si tu ndani ya Iran bali hata nje yake pia ambapo watu kwa kuzingatia utukufu wa mtu huu mpaka wamefikia kuchoma moto bendera za Marekani na Israel.

 

Aidha pia Ayatollah Khamenei katika kuzungumzia siku nyingine ya Mwenyezi Mungu, ameitaja siku ya majeshi ya Sepah kushambulia gome ya Marekani na kusema kuwa ukiachilia mbali mashambulio ya kimaada na kijeshi, kuna shambulio kubwa zaidi ambalo ni la kiroho na imani ya huyu mwenye kujiona mwamba. Huku akiashiria kwamba pigo hili ni kubwa zaidi hasa katika kuondoa hadhi na heshima ya Marekani, hadhi ambayo haitarudi hata kwa kuongezeka kwa vikwazo ambavyo vimetangazwa karibuni.

Ayatollah Khamenei pia ameashiria kuwa uwezo wa Mwenyezi Mungu kwa majeshi ya Sepah kuweza kushambulia ngome za Marekani, udhihiri wa watu kwa mamilioni katika musindikiza jeneza la Qasem Soleimani ni ishara ya utendaji wenye kumtegemea Mwenyezi Mungu kutoka kwa Jeshi la Sepah na kiongozi huyu mkubwa aliyeuliwa.

 Kauli yake kuhusu Mataifa ya Iran:

Aidha Ayatollah Khamenei katika hotuba yake ameashiria mbinu za mataifa ua Ulaya kutaka kuzima ukubwa wa masiku haya mazito, huku njia za kutaka kuchukua maswala ya nyuklia kama chambo ikiwa ndio kubwa mno kwa mataifa hayo.

“...Lakini tayari viongozi wetu wameshajibu majibu mazuri, na taifa linakumbuka vizuri sana katika miaka nane ya vita walivyokuwa wahami wakubwa wa Saddam dhidi ya Iran...” alisema Ayatollah Khamenei.

“....Tangu mwanzoni nilisema kuwa sina imani na maneno yamataifa ya Ulaya, hakuna wanachofanya kwani wote wapo katika kumtumikia Marekani, na sasa hivi imeshajulikana wazi kabisa ambapo kwa maana halisi tunaweza sema ni wadhaifu na misingi ya Marekani, wakiwa na dhana kwamba wanaweza kulifanya dhalili taifa la Iran, jambo ambalo hata mabwana na wakubwa wao Marekani pia hawawezi kufanya hivyo....” alitilia mkazo Ayatollah Khamenei.

Katika kukamilisha hotuba yake ya kwanza Ayatollah Khamenei ameashiria mambo kadhaa yakiwemo:

  • Umuhimu wa taifa la Iran kujizatiti na kwamba ndio njia pekee ya kulipa hadhi taifa lao.
  • Kwa baraka na uwezo wa Mwenyezi Mungu taifa la Iran siku hadi siku linakuwa, si tu katika uwanja wa kijeshi, bali hata kiuchumi, kielimu ambapo msingi wa haya yote ni kusimama katika utafutaji usio katika.
  • Kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu taifa la Iran si tu kwamba litakuwa mbali sana, bali itafikia hatua maadui hawatakuwa hata na uwezo na uthubutu wa kulitishia.

Tahadhari:

Aidha kabla ya hotuba ya pili Ayatollah Khamenei alitoa wito kwa raia wote kuhudhuria katika uchaguzi wao ambao atauongelea kwa kirefu masiku yajayo, lakini jambo la muhimu kutambua ni kwamba uchaguzi ndio msingi wa kusimama kwa nchi, nchi ambayo itawakatisha tamaa maadui wote.

Pia alitoa tahadhari yake kunako umakini wa watu katika kuliendea swala hili na kwamba wawe makini isije ikapatikana nafasi kwa adui kutimiza malengo yake.