Main Title

source : Parstoday
Jumamosi

16 Machi 2024

19:29:33
1444899

ICJ kuanza kusikiliza kesi ya mauaji ya kimbari inayoikabili Ujerumani Aprili

Majaji wa Mahakama ya Kimataifa ya Haki ICJ wamesema kesi iliyowasilishwa na Nicagarua ikiishtaki Ujerumani kwa kuunga mkono utawala wa Kizayuni katika mauaji ya kimbari ya Wapalestina itaanza kusikilizwa mwezi ujao wa Aprili.

Taarifa ya jana Ijumaa ya mahakama hiyo ya Umoja wa Mataifa yenye makao yake mjini The Hague nchini Uholanzi imesema, majaji wa korti hiyo ya kimataifa watafanya vikao vya kusikiliza pande zote kwenye kesi hiyo dhidi ya Ujerumani Aprili 8 na 9.

Wiki mbili zilizopita, Nicaragua ilizishitaki Ujerumani, Uingereza, Uholanzi na Canada katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki ICJ kwa kuunga mkono utawala wa Kizayuni katika mauaji yake ya kimbari ya Wapalestina.

Serikali ya Managua ilitangaza katika taarifa rasmi kwamba, Uingereza, Ujerumani, Uholanzi na Canada zinahusika katika ukiukaji mkubwa na wa kimpangilio wa Mkataba wa Kuzuia na Kutoa Adhabu kwa Uhalifu wa Mauaji ya Kimbari na Sheria za Kimataifa za Masuala ya Kibinadamu katika Ukanda wa Gaza.

Katika taarifa hiyo iliyotolewa na serikali ya Nicaragua, nchi nne za Ujerumani, Uingereza, Uholanzi na Canada zimetakiwa pia ziache kupeleka silaha, risasi na teknolojia za kijeshi kwa utawala wa Kizayuni.Majaji wa Mahakama ya Kimataifa ya Haki ICJ wamesema kesi iliyowasilishwa na Nicagarua ikiishtaki Ujerumani kwa kuunga mkono utawala wa Kizayuni katika mauaji ya kimbari ya Wapalestina itaanza kusikilizwa mwezi ujao wa Aprili.