Main Title

source : Parstoday
Jumapili

7 Aprili 2024

14:39:41
1449778

Qalibaf: Enzi ya ubabe wa Israel kwa himaya ya Marekani imekwisha

Spika wa Bunge la Iran Mohammad Baqer Qalibaf amesema enzi za ubabe wa utawala wa Isarel kwa himaya ya Marekani katika eneo la Asia Magharibi zimepita na utawala huo unaelekea kuangamia.

Qalibaf ameyasema hayo leo Jumapili katika kikao cha wazi cha Bunge mjini Tehran wakati utawala huo haramu unatekeleza jinai zinazokiuka sheria zote za kimataifa huku ukiwa umeshindwa kufikia malengo yake katika miezi sita ya vita vyake vya mauaji ya kimbari katika Ukanda wa Gaza.

Qalibaf ameongeza kuwa: "Kwa kulenga ubalozi mdogo wa Iran nchini Syria, adui ghasibu wa Kizayuni kwa mara nyingine tena amethibitisha kwamba hajui mipaka anapofanya jinai."  Aidha amesema utawala wa Israel  unachukiwa  duniani kutokana na kukiuka waziwazi kanuni zote za kimataifa.

Akiashiria shambulizi la utawala wa Isarel dhidi ya ubalozi mdogo wa Iran jijini Damascus, Qalibaf amesema kuwa taifa la Iran litatoa adhabu kali kwa Israel ambayo itaharakisha kusambaratika kwake.

Jumatatu iliyopita, mashambulizi ya anga ya utawala wa Israel yaliharibu jengo la ubalozi mdogo wa Iran katika mji mkuu wa Syria Damascus na kuua watu 13 wakiwemo maafisa saba wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC).

342/