Tukio hilo lilitokea majira ya saa mbili na robo usiku wa kuamkia jana Alkhamisi, nje ya ubalozi mdogo wa Israel ambao unakabiliana na Hoteli ya Four Seasons katikati mwa jiji la Boston.
Kulikuwa na idadi kubwa ya polisi eneo la tukio huku wapelelezi wakikusanya ushahidi na kupekua magari katika eneo hilo jana Alhamisi.
Walioshuhudia wameeleza kuwa, lilikuwa tukio la kuhuzunisha sana. Mtu huyo alipelekwa katika hospitali ya eneo hilo akiwa na majeraha ya moto, lakini hali yake ya kiafya haijajulikana.
Utambulisho wa mtu huyo, nia, na hali yake haijulikani kwa sasa, lakini hatua yake inatukumbusha Aaron Bushnell, ambaye alijitoa uhai mbele ya ubalozi wa Israel mjini Washington, DC mnamo Februari mwaka huu wa 2024 akipinga mauaji ya kimbari yanayoendelea kufanywa na Israel dhidi ya Wapalestina wa Ukanda wa Gaza.
Bushnell alikuwa akihudumu katika Kitengo cha 70 cha Ujasusi, Ufuatiliaji na Upelelezi wa Jeshi la Anga la Marekani, ambako inasemekana alifanya kazi kama "Fundi wa Huduma za Ubunifu."
Aaron Bushnell, alielekea katika ubalozi wa Israel mjini Washington ambako alijimwagia petroli kichwani na nguoni na kujichoma moto huku akikariri kwa sauti kubwa: “Palestina Huru, Palestina Huru” hadi alipokata pumzi. Rubani huyo shujaa mtetezi wa Wapalestina ambaye alisema kwa sauti kubwa kwamba hataki kushiriki tena katika mauaji ya kimbari, aliaga dunia baadaye. Kwa mujibu wa kumbukumbu za mafariki wa karibu wa Bushnell zilizochapishwa katika tovuti ya Crimethinc, askari huyo wa Jeshi la Anga la US aliandika wosia akitaka majivu na maiti yake yamiminwe katika ardhi ya Palestina.
Alisema kwenye wosia huo kuwa, "Iwapo muda utafika Wapalestina wadhibiti tena ardhi yao, na pia iwapo watu asilia wa ardhi hiyo (Palestina) wataafika wazo langu, ningelipenda majivu yangu yasambazwe katika Palestina iliyo huru."
342/