Sigrid Kaag, ambaye aliteuliwa miezi tisa iliyopita kuboresha utoaji wa misaada inayohitajika haraka, jana Jumatatu alitarajiwa kutoa ripoti kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Alielezea hali katika eneo hilo kama "janga kubwa". "Hatukidhi mahitaji, achilia mbali kujenga matarajio na matumaini kwa raia wa Gaza."
Mratibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Utekelezaji wa masuala ya kibinadamu na Ujenzi mpya huko Gaza amesema kuwa, mifumo ya kutoa msaada, ikiwa ni pamoja na njia nyingi za ardhini na baharini hadi Gaza sasa iko tayari.
Aidha amesema kuwa, Umoja wa Mataifa unafanya kazi usiku na mchana na watu wanahatarisha maisha yao siku hadi siku".Lakini amelitaja eneo la Gaza kuwa, "mahali pasipo salama zaidi duniani kufanya kazi". Alisema anasikitika kwamba "hakuna mengi zaidi yanayoweza kuboreshwa" hadi kuwe na usitishaji mapigano na kuachiliwa kwa mateka wa Israeli bado wanazuiliwa huko.
Hayo yanajiri katiika hali ambayo, ripoti mpya ya Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa Duniani WHO imebaini kwamba kwamba takriban robo ya Wapalestina waliojeruhiwa katika vita vya mauaji ya kimbari vya Israel dhidi ya Gaza ambao ni sawa na watu 22,500 wanakabiliwa na majeraha ya kubadilisha maisha ambayo yanahitaji huduma za marekebisho sasa na kwa miaka ijayo.
342/