Main Title

source : Parstoday
Jumapili

29 Septemba 2024

18:17:04
1489798

Lavrov: Mauaji ya Nasrullah yana lengo la kuchochea vita vya Marekani na Iran

Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia, Sergey Lavrov, anasema kwamba mauaji ya Israel dhidi ya Katibu Mkuu wa Hizbullah, Sayyid Hassan Nasrullah, huenda yalikusudiwa kuzusha vita kati ya Marekani na Iran.

Lavrov aliwaambia waandishi wa habari katika mkutano na waandishi wa habari baada ya kuhutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York kwamba watu wengi wanaamini kwamba, mauaji ya Israel dhidi ya Sayyid Hassan Nasrullah yalilenga kuichokoza Iran na Marekani "kuanzisha vita kamili katika eneo zima la Magharibi mwa Asia."

"Kumuua kiongozi wa Hizbullah haikuwa tu mauaji ya kisiasa. Ni kitendo cha kijinga sana", amesema Lavrov.

"Watu wengi wanasema - kwamba Israel inataka kujenga misingi ya kuivuta Marekani moja kwa moja katika vita, inajaribu kuichokoza Iran," Lavrov ameongeza.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia amesema: "Uongozi wa Iran, una tabia ya kuwajibika sana. Hili ni jambo ambalo tunapaswa kuzingatia."

Akizungumza katika mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa siku ya Ijumaa, Lavrov alisema, "Kwa mara nyingine tena Mashariki ya Kati iko ukingoni mwa vita vikubwa," akitoa wito wa kufanyika juhudi za kidiplomasia kuzuia "hali mbaya zaidi."

342/