Main Title

source : Abna
Jumatano

9 Oktoba 2024

09:45:46
1493095

Siku ya Tatu ya Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani Malaysia

Siku ya tatu ya mashindano ya 64 ya kimataifa ya Qur'ani ya Malaysia ilishuhudia washindani tisa katika kitengo cha qiraa wakipanda jukwani katika ukumbi wa Kituo cha Biashara Duniani jijini Kuala Lumpur siku ya Jumatatu.

Qari wa Kazakhstan Ahmet Serik aliongoza orodha ya washiriki, akifuatiwa na qari wa Kanada Mhammad Maruf Hssain na qariah wa India Sumayya Sadia.

Wengine walioshiriki katika usiku wa tatu ni Wahyu Andi Saputra kutoka Indonesia, Ahmet Redzematovic kutoka Montenegro, Rumaisa Abdul Rashid kutoka Pakistan, Abdullah Soe Min Htike kutoka Myanmar, Raihana Ambangala kutoka Ufilipino, na Muhammad Baqir Shahul Hameed kutoka Hong Kong.

Asubuhi, washiriki 10 katika kitengo cha kuhifadhi walipanda jukwani.

Jumla ya wasomaji na wahifadhi 92 kutoka nchi 71 wanashiriki katika mashindano hayo yanayojulikana kwa jina la Majlisi ya Kimataifa ya Kuhifadhi na Kuhifadhi Qur'ani ya Malaysia (MTHQA).

Ni pamoja na wahifadhi 53 wa na maqari 39 wa Qur’ani.

Sherehe ya kufunga mashindano hayo yaliyoanza Oktoba 5 itafanyika Oktoba 12 ambapo waloshika nafasi za juu watatunukiwa zawadwashindi wakuu watatangazwa na kutunukiwa imepangwa kufanyika Oktoba 12.

IQNA