Akihutubia halaiki kubwa ya Waumini katika Uwanja wa Chuo Kikuu cha Tehran, Ayatullah Imami Kashani ameongeza kuwa badala ya kuomba msamaha, utawala wenye kiburi wa Marekani sasa unataka urejeshewe ndege hiyo ya kijasusi.Ayatullah Mohammad Imami Kashani ametaka mataifa ya dunia hasa taifa la Marekani lijibu swali hili kuwa je, hatua ya ndege ya kijasusi ya kuingia kinyume cha sheria katika anga ya nchi nyigine ni uhalifu au la? Amehoji pia ni kwa nini sheria za kimataifa zinakiukwa kwa kiwango hiki. Akihutubia halaiki kubwa ya waumini katika uwanja wa Chuo Kikuu cha Tehran, Ayatullah Kashani ameashiria kipengee cha pili ibara ya nne ya Chata ya Umoja wa Mataifa inayosema kukiuka mamlaka au uhuru wa kisiasa wa nchi ni jambo ambalo linaenda kinyume na sheria za kimataifa na hutambuliwa kama hujuma dhidi ya nchi huru. Kashani amesema Marekani inatumia vibaya uwezo wake wa kisayansi na kusababisha umwagikaji damu duniani. Amesema unyama na ukatili wa Marekani unawatia wasiwasi mkubwa walimwengu. Ayatullah Imami Kashani pia ameashiria kupitishwa maazimio 9 dhidi ya utawala wa Kizayuni katika Umoja wa Mataifa na kusema maazimio hayo yemevunja ndoto ya utawala ghasibu wa Israel ya kuteka zaidi ardhi za Wapalestina.
19 Machi 2011 - 20:30
News ID: 284442
Khatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran amelaani hatua ya ndege ya kijasusi ya Marekani ya kukiuka anga ya Iran na ametaka Washington iiombe Iran msamaha rasmi baada ya ndege hiyo kunaswa nchini.