Kikao hicho kilichofanyika Makao Makuu ya JMAT-TAIFA kililenga kuweka mikakati na kufanya maandalizi ya mwisho kuelekea Kongamano Kuu la Qur'an litakalofanyika kesho, Mei 20, 2025, katika Ukumbi wa Mikutano ya Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC), Dar es Salaam.
Kongamano hilo linatarajiwa kuanza saa 8:00 Mchana hadi saa 11:00 Jioni, na litajumuisha washiriki kutoka sehemu mbalimbali za nchi pamoja na wageni maalum kutoka ndani na nje ya Tanzania.
Wito umetolewa kwa wananchi wote, hasa wapenzi wa Qur'an na wadau wa amani, kuhudhuria kwa wingi ili kufanikisha azma ya kueneza mafundisho ya Qur'an na kuimarisha misingi ya maridhiano katika jamii.
Your Comment