Main Title

source : abna.ir
Alhamisi

24 Julai 2014

09:20:32
626332

Siku ya Quds

siku ya Quds ni siku ya kimataifa ya utetezi wa raia madhulumu wa Parestina.

siku ya Quds ni siku ya kimataifa ya utetezi wa raia madhulumu wa Parestina.
Baada ya Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran hayati Ruhullah Khomeini aliitangaza Ijumaa ya mwisho ya kila mwezi wa Ramadhani kuwa siku ya Kimataifa ya Quds kwa minajili ya kuwatetea wananchi wanaokandamizwa Wapalestina.
Imam Khomein (r.a) mnamo Ramadhan 1399 B.H. sawa na Augosti 1979 alisema: Nawaita Waislamu ulimwenguni pote kutukuza Ijumaa ya mwisho ya mwezi mtukufu wa Ramadhan kama ‘Siku ya Quds’ na kutangaza mshikamano wa Waislamu katika kuunga mkono haki halisi za Waislamu wa Palestina.
wito huu wa kiongozi muadhamu wa mapinduzi ya kiislamu ya Iran, umepokewa kwa nguvu zote na ulimwengu mzima, ambapo siku hii ilianza kwa raia wa Iran na hatimaye imekuwa ni siku ya kimataifa.
wananchi na wapenda amani duniani kote katika kila Ijumaa ya mwisho ya mwezi mtukufu wa Ramadhan wanaandamana, kuelezea na kutoa msaada wao kwa wananchi madhulumu wa Parestina.
inasadikiwa kuwa Ijumaa ya kesho ya Quds day kutakuwa na maandamano makubwa zaidi ya yale ya miaka iliyopita hii inatokana na kuwa sanjari na mashambulizi ya Israel dhidi ya raia wa Gaza Parestina.