Changamoto
-
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Akutana na Naibu Mkuu wa Baraza Kuu la Kishia Lebanon Beirut
Wakati wa ziara yake rasmi mjini Beirut, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Seyyed Abbas Araghchi, alikutana na Sheikh Ali Al-Khatib, Naibu Mkuu wa Baraza Kuu la Kiislamu la Kishia nchini Lebanon. Mazungumzo yao yalijikita katika maendeleo ya kikanda, umuhimu wa umoja wa Kiislamu, na kuimarisha ushirikiano wa kidini na kisiasa kwa ajili ya uthabiti na mshikamano wa Lebanon.
-
Walinzi wa mipaka wa Iran waliweza kuokoa zaidi ya raia 2,000 wa Afghanistan waliokumbwa na theluji nzito na hali ya baridi kwenye mipaka
Operesheni hii ya kuokoa maisha ilifanyika chini ya hali ngumu za hewa na baridi kali, ambapo walinzi wa mipaka kwa ushirikiano na vikosi vya dharura waliweza kuwatokomeza watu waliokumbwa na hatari ya kifo kutokana na baridi na theluji katika maeneo ya milima yenye changamoto kubwa ya kufikika.
-
Mwanachama wa Jumuiya ya Walimu wa Qum atoa wito wa umoja wa wanazuoni na wasomi kwa ajili ya kufanikisha ustaarabu mpya wa Kiislamu
Hujjatul Islam wal Muslimin Muhammad Saeed Waezi amesema kuwa kuimarisha umoja na mashauriano kati ya wanazuoni na wasomi wa Kiislamu ni jambo muhimu katika kukabiliana na changamoto za sasa na kufikia malengo makubwa ya ustaarabu mpya wa Kiislamu.
-
Wazayuni Wajibu Kauli za Trump: “Sisi Hatuko Chini ya Utawala wa Marekani!”
Hali ya sasa ya utawala wa Kizayuni (Israel) kutokana na utegemezi wake mkubwa kwa siasa za Marekani pamoja na changamoto za ndani, imegeuka kuwa moja ya hatua muhimu za kihistoria katika uhusiano wa kimataifa wa utawala huo. Mabadiliko haya yanaweza kusababisha mabadiliko ya kimkakati katika siasa za Israel na namna inavyoshirikiana na jamii ya kimataifa na Wapalestina.
-
Araqchi: Taliban Haijaheshimu Haki za Waislamu wa Kishia wa Afghanistan
Ikumbukwe kuwa, baada ya kurejea madarakani, Taliban ilifuta rasmi Sheria ya Hali ya Kiraia ya Waislamu wa Kishia, na kuondoa vitabu vyote vya Fiqh ya Ja’fari kutoka vyuo vikuu, shule na maktaba za serikali. Kundi hilo limekuwa likisisitiza kwamba sheria za Afghanistan lazima zitekelezwe kwa mujibu wa Fiqh ya Kihanifi pekee.
-
Mufti wa Tanzania, Sheikh Dkt. Abubakar Zuber, Arejea Nchini Baada ya Kikao cha Kimataifa Nchini Misri
"Tumejadili namna bora ya kumaliza mzozo huo kwa njia ya amani. Na tunawaombea ndugu zetu wa Gaza ili Mwenyezi Mungu awape amani na kumaliza mgogoro huu wa muda mrefu,"
-
Baada ya kusaini makubaliano makubwa zaidi ya nishati katika historia yake - Je, Afghanistan inakaribia kujitegemea?
Kabul imeanza safari ya kuzalisha megawati 10,000 za umeme baada ya kusaini makubaliano makubwa zaidi ya nishati katika historia yake, mpango unaoweza kuibadilisha kutoka nchi inayoagiza umeme hadi kuwa muuzaji wa nishati katika ukanda.
-
Chuo Kikuu cha Jamiatul Mustafa - Dar-es-salaam - Tanzania kimeandaa Kongamano la Kisayansi kuhusu Maendeleo katika Ulimwengu wa Kiislamu
Kongamano hili litajadili juu ya Maendeleo katika Ulimwengu wa Kiislamu kati ya changamoto na mkakati. Mhadhiri: Samahat Sheikh Mulaba Saleh. Siku ya: Jumamosi; 19/04/2025. Kuanzia: 10 - 12:00 AM. Katika Ukumbi wa Sala wa Chuo cha Jamiat Al- Mustafa. Watu wote mnakaribishwa kuhudhuria katika nad'wa hii ya Kisayansi.