Chama cha Hizbullah kimetoa tamko kali kupinga uamuzi mpya wa serikali inayoongozwa na Nawaf Salam, ambao wanauona kama hatua ya hatari ya kudhoofisha muqawama (mapambano ya ukombozi) na kukabidhi usalama wa Lebanon kwa Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel. Katika taarifa hiyo, Hizbullah imesisitiza kuwa itakabiliana na uamuzi huu kwa msimamo thabiti kama hatua isiyokubalika kabisa, huku ikisisitiza umuhimu wa kulinda silaha za kujihami na kuimarisha jeshi la taifa kwa ajili ya kutetea ardhi na uhuru wa Lebanon.
Lebanon Bado Chini ya Vitisho vya Israel na Marekani