Waziri Mkuu wa Malaysia amelaani uchokozi wa kijeshi wa Marekani na utawala wa Kizayuni dhidi ya Iran, akisema kuwa msimamo, azma na uvumilivu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika kukabiliana na mashambulizi hayo unastahili pongezi.
Iran na Oman zimesisitiza umuhimu wa kutumia fursa ya sasa ya kidiplomasia kuunga mkono amani, kupunguza mvutano na kuimarisha utulivu kwa kuzingatia sheria za kimataifa na ujirani mwema.