Kwenye nyuma ya pazia ya mabadiliko haya, Marekani na Israel kwa vitendo wanaandaa mfumo wa kisiasa na kiusalama ambao lengo lake kuu ni kumaliza uwepo wa vikosi vya upinzani kwenye mipaka ya kusini.
Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon, katika hotuba ya kumbukumbu ya mashahidi Sayyid Hassan Nasrallah na Sayyid Hashim Safiuddin, amesisitiza kuwa Hizbullah imesalia thabiti katika ahadi yake na itapinga vikali jaribio lolote la kuondoa silaha zake.
Serikali ya Taliban imejibu kauli za Donald Trump kuhusu kurejesha kambi ya Bagram kwa kusema kuwa uwepo wa kijeshi wa Marekani nchini Afghanistan ni jambo lisilowezekana kabisa.