Wageni
-
Maulid ya Kitaifa 2025 Yang'ara Tanga | Rais wa Jamiat al-Mustafa (s) - Tanzania Sh.Dr. Ali Taqavi Ajumuika na Umma Kuadhimisha Maulid ya Mtume (saww)
Sherehe hiyo ya Mazazi ya Mtume wa Ummah (saww), imeonesha mshikamano, mapenzi ya dhati, na hamasa kubwa ya waislamu katika kuenzi maisha na mafundisho ya Mtume Muhammad (s.a.w.w). Idadi kubwa ya washiriki katika hafla hii imekuwa ishara tosha ya mafanikio makubwa ya tukio hilo takatifu, na ushahidi wa mapenzi ya kweli kwa Mtume wa Mwisho
-
Ushiriki wa Vikundi vya Jihadi na Wananchi katika Mahema ya RASHT hadi Mwisho wa Mwezi wa Safar
Kamanda wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi (SEPAH) wa Eneo Kuu la RASHT, Kanali Hassan Amini, ametangaza kuhusu kuanzishwa kwa mahema ya wananchi katika barabara ya watembea kwa miguu ya kiutamaduni ya Manispaa ya Rasht kwa mwaka wa nne mfululizo, na kusema kuwa mahema haya, yenye programu za kitamaduni, huduma na kidini, yatapokea wageni na wapenzi wa Sayyid al-Shuhadaa (a.s.) hadi mwisho wa mwezi wa Safar.
-
Makamu wa Rais wa Baraza Kuu la Kiislamu la Kishia Lebanon Aikosoa Vikali Serikali ya Nchi Hiyo
Alielekeza maneno yake kwa Rais Joseph Aoun, akisema: "Uliwaambia watu wa Muqawama kuwa waitegemee Serikali – lakini haukusema ni Serikali ipi hiyo? Watu wetu hawako tayari kuwa wahanga wa wauaji ambao watawatendea kama walivyowatendea Wapalestina."
-
Ripoti ya Mahudhurio ya Wasomaji wa Qur'an wa Programu ya "Mahfali" nchini Tanzania
Katika hafla hii Tukufu ya Qur’an, wasomaji wa Kiirani walioshiriki ni pamoja na Ustadh Shakernejad, Ustadh Abolghasemi, Qari kijana Mohammad Hossein Azimi, na Muhanna Ghanbari – ambaye ni mhifadhi wa Qur’an nzima.