siri
-
Mjumbe wa Baraza la Wanazuoni wa Kiislamu nchini Bahrain:
Hukumu za Kisiasa Dhidi ya Wanazuoni wa Kishia Zimeandaliwa Mapema; Kesi Zinaendeshwa kwa Njia Zisizo za Haki na kwa Usiri
Sheikh Muhammad Khujasta, akipinga mwenendo wa kesi zinazowakabili wanazuoni wa Kishia nchini Bahrain, amesisitiza kuwa hukumu zinazotolewa dhidi ya wanazuoni hao zimeamuliwa mapema. Ameeleza kuwa lengo la mchakato huo si kuwahukumu viongozi wachache wa dini pekee, bali ni kukandamiza jamii nzima ya Kishia.
-
Kikao cha Siri cha Netanyahu Abu Dhabi; Hofu ya Bab al-Mandab Kurudi Chini ya Udhibiti wa Yemen
Kufuatia Yemen kurejesha kikamilifu mamlaka yake juu ya Mlango wa Bahari wa Bab al-Mandab na maeneo ya pwani ya magharibi, Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa utawala wa Israel, alifanya ziara ya siri na ya dharura mjini Abu Dhabi, ambapo alishiriki katika kikao cha siri kilichowahusisha wawakilishi wa nchi kadhaa za Kiarabu, zikiwemo Saudi Arabia, Jordan na Morocco, pamoja na wawakilishi wa vikosi vinavyomuunga mkono Khalifa Haftar nchini Libya. Lengo la kikao hicho limetajwa kuwa ni kuunda muungano wa kijeshi wa kujihami utakaokuwa mbadala, kwa ajili ya kufidia kushindwa kwa vikosi hivyo katika uwanja wa vita na kusambaratika kwa muungano unaoongozwa na Saudi Arabia.
-
Majibu kwa Shubuhati Zinazohusu Wilayat na Uimamu, na Siri Iliyofichika katika Tukio la Ghadir
«وَلَوْ شِئْتُ أَنْ أُسَمِّیَ الْقَائِلِينَ بِذَلِكَ بِأَسْمَائِهِمْ لَسَمَّيْتُ ... وَلَكِنِّي وَاللَّهِ فِي أُمُورِهِمْ قَدْ تَكَرَّمْتُ» "Na kama ningetaka kuwataja wale waliotoa maneno hayo kwa majina yao, basi ningewataja. Lakini kwa hakika, kwa jina la Mwenyezi Mungu, nimewatendea kwa ukarimu na staha katika mambo yao." Kauli hii inaonyesha kwamba Mtume (s.a.w.w.) aliwajua wanafiki mmoja baada ya mwingine na alikuwa na uwezo wa kuwataja waziwazi. Hata hivyo, kutokana na hekima, ukarimu na maslahi ya Umma wa Kiislamu, hakufanya hivyo. Je, jambo hili lina maana kwamba Mtume (s.a.w.w.) alipuuza wajibu wake? Hapana. Kusudi la utume halikuwa tu kufichua watu, bali lilikuwa kuongoza jamii, kuwapa nafasi ya kutubia na kurejea katika haki, pamoja na kulinda umoja wa Waislamu dhidi ya fitina kubwa zaidi. Kama Mtume (s.a.w.w.) angewataja wanafiki wote hadharani, huenda baadhi yao wangetangaza uasi wao dhidi ya Uislamu, jambo ambalo lingeweza kusababisha migawanyiko mikubwa na hata vita vya ndani katika jamii changa ya Kiislamu. Kwa hiyo, kunyamaza kwake kuhusu majina yao hakukuwa udhaifu wala kuacha wajibu, bali ilikuwa ni sehemu ya hekima ya uongozi wa Mtume katika kuhifadhi maslahi makubwa ya dini na jamii.
-
Imam Ali (a.s) na Siri za Ukuruba Wake kwa Mtume Mm Muhammad (s.a.w.w)
Imam Ali (a.s) si tu sahaba wa karibu wa Mtume (s.a.w), bali ni zao la malezi ya moja kwa moja ya Mtume, shahidi wa mwanzo wa wahyi, na mhimili wa maadili ya Kiislamu. Upendo na ufuasi wake unabaki kuwa kipimo muhimu cha uaminifu wa kweli kwa Uislamu na Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w).
-
Mbunge wa Lebanon;
Afichua kuhusu Mpango wa Kuangamiza Silaha za Muqawama / Hakuna Uthibitisho wa Safari ya Afisa wa Mahusiano ya Kigeni wa Hezbollah kwenda Saudi Arabia
Ikumbukwe kuwa jarida moja la Lebanon lilidai hivi karibuni kuwa Ammar Al-Moussawi, afisa wa mahusiano ya kigeni wa Hezbollah, amekuwa kwa siku tatu katika safari ya siri nchini Saudi Arabia kwa upatanishi wa Uturuki, madai ambayo hadi sasa hayajathibitishwa rasmi.
-
Kufichuliwa kwa muundo wa siri wa utawala wa Kizayuni kwa ajili ya kukwepa uwajibikaji / Haki iko chini ya upanga wa fedha na nguvu ya utawala
Tovuti ya Kifaransa Mediapart, kwa ushirikiano na vyombo vingine nane vya habari vya Ulaya, kupitia mradi unaoitwa “Faili za Utawala wa Kizayuni”, imefichua kuundwa kwa kitengo cha siri ndani ya Wizara ya Sheria ya utawala huo.
-
Nakuru - Kenya | Khatibu wa Sala ya Ijumaa Sheikh Abdul Ghani Khatibu Aeleza Siri ya Utukufu wa Bibi Fatima (sa) kupitia Hadithi Tukufu za Mtume(saww)
Sheikh Abdul Ghani aliweka wazi kuwa mapenzi ya Mtume (saww) kwa Bibi Fatima (sa) hayawezi kuchukuliwa kwa mtazamo wa kawaida wa mapenzi ya baba kwa binti yake. Badala yake, ni tamko la kiungu na kijamii linalobainisha nafasi yake adhimu katika Uislamu.
-
Darsa Fupi na Muhimu Katika Muktadha wa Maombolezo ya Bibi Fatimah az-Zahra (a.s) kuhusu "Fadhila na Siri za Tasbihat az-Zahra (a.s) na Ayatul Kursi"
Imam al-Baqir (a.s.) amesema: “Anayesema Tasbih ya Fatimah az-Zahra (a.s.) kisha akaomba maghfirah, atasamehewa. (Tasbih hiyo inaposomwa na mja) Ni mia moja kwa ulimi wake, lakini ni elfu moja katika mizani.”