tishio
-
Mwanasayansi wa Nyuklia wa Lebanon katika mazungumzo na ABNA:
Kuangamiza mpango wa nyuklia wa Iran ni ndoto / Tishio la kijeshi la Marekani dhidi ya Iran lina gharama kubwa kuliko uwezo wa Washington
Mkuu wa Kituo cha Ushauri wa Kimkakati cha Usalama wa Nishati ya Nyuklia nchini Lebanon amesisitiza kuwa Marekani—hasa katika kipindi cha Donald Trump—haina nia ya kuingia katika vita hatari dhidi ya Iran, huku Israel ikijaribu kuibebesha Washington mzigo wa gharama za makabiliano hayo.
-
Mkutano wa dharura wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu kujadili na kukabiliana na mradi wa Israel kuhusu Somalia
Jumuiya ya Nchi za Kiarabu, katika mkutano wa dharura uliofanyika leo Jumapili nchini Misri, imeitikia hatua ya utawala wa Kizayuni wa Israel ya kulitambua eneo la Somaliland, na ikaeleza kuwa hatua hiyo ni tishio kwa usalama wa kikanda na ni ukiukaji wa wazi wa sheria za kimataifa.
-
Turki Al-Faisal: Tishio Kuu la Mashariki ya Kati Sio Iran, Bali ni Israel
Shambulizi Dhidi ya Ujumbe wa Hamas Qatar ni Onyo kwa Nchi za Ghuba | Katika kauli yake nzito, Turki Al-Faisal pia amebainisha kuwa shambulizi la Israel dhidi ya ujumbe wa Hamas nchini Qatar lilikuwa ujumbe wa vitisho kwa nchi za Ghuba, akisema hatua hiyo ilikuwa onyo la wazi kuwa mataifa ya Ghuba yako katika hatari na yanapaswa kuchukua tahadhari za pamoja za kiulinzi.
-
Iran: Kukabiliana na ugaidi kunahitaji ushirikiano wa kikanda, hasa na Afghanistan
Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran alitangaza kuwa makundi ya kigaidi hayapo tu nchini Afghanistan, bali yameenea katika nchi mbalimbali za eneo hilo. Alisisitiza kuwa kukabiliana na tishio hili kunahitaji ushirikiano wa pamoja wa nchi jirani, hasa Afghanistan.
-
Abdulmalik al-Houthi: Mpango wa Kuvinyang’anya Silaha Vikundi vya Muqawama ni wa Kipuuzi na Unahudumia Maadui
“Lau Umma wa Kiislamu ungetilia mkazo tangu mwanzo juu ya ujenzi wa jeshi la Kipalestina lenye nguvu, hali ya leo isingekuwa kama ilivyo.”
-
Sheikh al-Azhar, Ahmad al-Tayeb, amelaani vikali mashambulizi ya uchokozi ya Israel dhidi ya Iran
Kimya cha jumuiya ya kimataifa kuhusu uonevu na uchokozi huu na kukosekana kauli za kuuzuwia, kinachukuliwa kuwa ni ushiriki katika jinai hizo, na matokeo yake pekee yatakuwa ni tishio kwa usalama wa dunia nzima. Vita havizai amani."