Main Title
29 Machi 2024
Watu 38 wauawa katika hujuma za anga za Israel Syria, Iran yalaani
Kwa akali watu 38 wameuawa katika mashambulizi ya anga ya utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya mji wa Aleppo (Halab) huko kaskazini mwa Syria.
29 Machi 2024
HAMAS: Misimamo ya Israel imekwamisha mazungumzo ya Doha
Mmoja wa viongozi waandamizi wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema mazungumzo ya kusimamisha vita katika Ukanda wa Gaza yamegonga mwamba huko Doha, mji mkuu wa Qatar kutokana na misimamo isiyoeleweka ya utawala haramu wa Israel.
28 Machi 2024
Ireland 'kuingilia kati' kesi ya mauaji ya kimbari ya Afrika Kusini dhidi ya Israel
Ireland imetangaza kwamba "itaingilia" katika kesi ya mauaji ya kimbari iliyoanzishwa mwishoni mwa mwaka jana na Afrika Kusini katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) dhidi ya utawala wa Israel, kutokana na vita vya miezi kadhaa vya mauaji ya halaiki kwenye Ukanda wa Gaza.
28 Machi 2024
Ripota wa UN: Nilitishwa kwa sababu ya ripoti yangu kuhusu mauaji ya kimbari huko Gaza
Ripota Maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu katika ardhi za Palestina, Francesca Albanese, amesema kuwa amekuwa akikabiliwa na mashambulizi na kupokea vitisho vingi tangu alipoanza kazi yake ya kuandaa ripoti kuhusu jinai zinazofanywa na Israel katika Ukanda wa Gaza.
28 Machi 2024
Kaboni nyeusi; sio tu inachafua mazingira, lakini pia inasababisha ongezeko la joto duniani
Kaboni nyeusi imetajwa kusababisha ongezeko la joto kwa wati zisizopungua 0.6 kwa kila mita mraba moja katika uso wa dunia. Haya yamebainishwa na Mhadhiri wa masuala ya uhandisi wa mazingira katika Chuo Kikuu cha Istanbul Uturuki.
28 Machi 2024
Putin: 'Ni upuuzi tu' kudai kwamba Russia inapanga kuishambulia kijeshi NATO
Rais Vladimir Putin wa Russia amesema, nchi yake haina nia ya kuingia kwenye makabiliano ya kijeshi na vibaraka wa Marekani wa Ulaya Mashariki.
28 Machi 2024
UN: Khumsi moja ya chakula duniani inaishia jaani wakati watu milioni 783 wanalala na njaa
Ripoti mpya ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira UNEP imesema, wakati theluthi moja ya watu duniani wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula, milo bilioni moja, ambayo ni sawa na moja ya tano ya chakula chote hutupwa kila siku na kuishia jalalani.
28 Machi 2024
Wataalamu wa US: Mapigano ya Al-Shifa yanaonyesha wapiganaji Wapalestina wangali wako imara
Wataalamu wa masuala ya vita wa Marekani wamesema, wapiganaji wa Kipalestina wamefanya mashambulizi yapatayo 70 dhidi ya wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel karibu na hospitali ya al-Shifa katika mji wa Ghaza tangu Machi 18 wakati jeshi la utawala huo ghasibu liliporejea katika eneo hilo.
28 Machi 2024
Marekani yaiwekea vikwazo GAZA NOW kwa tuhuma za kuchangisha fedha za kuisaidia HAMAS
Wizara ya Fedha ya Marekani imeiwekea vikwazo tovuti ya mtandao ya GAZA NOW kwa madai ya kuchangisha misaada ya kifedha kwan ajili ya Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS.
28 Machi 2024
Rais wa Iran: Palestina sasa ni kadhia ya ulimwengu wa ubinadamu
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kutokana na muqawama au mapambano ya Kiislamu na misimamo imara ya wananchi wanaodhulumiwa na wenye nguvu wa Gaza, kadhia ya Palestina sasa imevuka mipaka ya ulimwengu wa Kiislamu na kuwa suala la ulimwengu wa ubinadamu.
28 Machi 2024
Msisitizo wa Iran juu ya haki yake katika medani ya gesi ya Arash
Naibu Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Masuala ya Sheria, Mohammed Dehghan, amesisitiza kuwa Jamhuri ya Kiislamu haitafumbia jicho kwa hali yoyote ile haki zake katika medani ya pamoja ya gesi ya Arash na haitaruhusu upande wowote kukiuka sheria za kimataifa katika suala hili.
28 Machi 2024
Marekani imeshindwa kukabiliana na jeshi la Yemen katika Bahari Nyekundu
Viongozi wa Marekani wamekiri kutokuwa na uwezo wa kukabiliana na jeshi la Yemen katika Bahari ya Shamu. Hii ni kufuatia kuendelea makablinao ya Magharibi chini ya uongozi wa Marekani dhidi ya jeshi la Yemen katika Bahari Nyekundu.
28 Machi 2024
Subira ya kihistoria ya watu wa Ghaza, sababu kuu ya kufedheheka Israel duniani
Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kwenye mazungumzo yake na Ismail Hania, Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS kwamba, subira ya kihistoria na kusimama imara wananchi wa Ghaza mbele ya jinai za utawala wa Kizayuni kumeifanya kadhia ya Palestina kuwa suala kuu nambari moja duniani.
28 Machi 2024
CAIR: UN ichunguze jeshi la Israel lilivyowaua Wapalestina bila sababu na kuzifukia maiti zao
Baraza la Mahusiano ya Kiislamu Marekani [CAIR] limetoa wito kwa Umoja wa Mataifa kuchunguza video inayoonyesha wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel wakiwapiga risasi bila sababuu Wapalestina wawili wanaoonekana kuwa hawana silaha kisha kuzifukia maiti zao kwa buldoza.
27 Machi 2024
Moscow: EU imekiri kuwa inahudumia ubeberu wa Marekani
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia amesema matamshi ya karibuni ya Josep Borrell, Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya ni ungamo la Magharibi kwamba inajihusisha na mgogoro wa Ukraine ili kuisaidia Marekani kudumisha nafasi yake ya ubeberu duniani.
27 Machi 2024
Soda ya 'Palestine Cola' yazinduliwa, mashirika ya Magharibi yaendelea kususiwa
Ndugu wawili wa Kipalestina wamezindua soda waliyoipa jina la 'Palestine Cola' na kusema kuwa, faida zote zitakazotokana na mauzo ya kinywaji hicho zitawaendea Wapalestina.
27 Machi 2024
Ulimwengu waunga mkono ripoti ya UN kuhusu mauaji ya kimbari ya Israel Ukanda wa Gaza
Tathmini iliyofanywa na Ripota Maalumu wa Umoja wa Mataifa katika Masuala ya Palestina ambayo imezitaja jinai za utawala wa Kizayuni huko Ukanda wa Gaza kuwa ni mauaji ya kimbari imeungwa mkono pakubwa na nchi mbalimbali katika umoja huo.
27 Machi 2024
Kutolewa pendekezo la kuanzisha klabu ya nyuklia ya BRICS kwa kuishirikisha Iran
Mkutano wa 13 wa kimataifa wa Atomexpo 2024 huko Sirius, Russia umetoa pendekezo la kuasisi klabu ya nyuklia ya nchi wanachama wa kundi la BRICS kwa kuishirikisha Iran.
27 Machi 2024
Wachunguzi wa Russia kujadili ombi la kuchunguza kuhusika Magharibi katika ugaidi
Wachunguzi wa serikali ya Russia leo wameeleza kuwa watajadili ombi lililowasilishwa na wabunge waliotaka kuchunguzwa kile walichokiita kama "taasisi, ufadhili na vitendo vya ugaidi vinavyofanywa na Marekani na nchi nyingine za Magharibi dhidi ya Russia."
27 Machi 2024
"Siku ya Quds imebakisha hai kadhia ya Palestina"
Mkuu wa Makao Makuu ya Intifadha na Siku ya Quds ya Iran amesema maandamano ya Siku ya Kimataifa ya Quds yana umuhimu mkubwa katika kubakisha hai kadhia ya ukombozi wa Palestina.