Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Sayyid Abbas Mousavi amesema hayo leo Jumatatu mbele ya waandishi wa habari na huku akigusia madai ya Robert O'Brien, mshauri wa usalama wa taifa wa rais wa Marekani aliyedai kuwa Iran inahusika katika machafuko yanayoendelea hivi sasa nchini Marekani amesema, maandamano na machafuko yanayoshuhudiwa hivi sasa huko Marekani ni matokeo ya miaka mingi ya dhulma na kukandamizwa kupindukia sauti ya wananchi na raia wa Marekani, hivyo viongozi wa Marekani wameshindwa na la kufanya zaidi ya kupayuka na kutoa madai yasiyo na msingi.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amewatumia ujumbe wananchi wa Marekani akisiwaambia, dunia imesikia kilio chenu cha kudhulumiwa na iko pamoja nanyi. Vile vile ameiasa serikali na polisi ya Marekani kwa kusema, acheni kutumia mabavu dhidi ya wananchi wenu, waacheni wapumue.
Aidha ameashiria hatua ya Iran ya kupeleka meli za mafuta nchini Venezuela na kuvunja vikwazo vya Marekani kwa nchi hiyo ya Amerika ya Latini akisema, Iran na Venezuela zimewekewa vikwazo vya kidhulma na Marekani, na hakuna nchi yoyote duniani yenye wajibu wa kuheshimu vikwazo hivyo kama ambavyo pia Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ina msimamo imara wa kulinda haki zake hata katika maeneo ya mbali.