18 Novemba 2020 - 15:33
Gharibabadi amhutubu Adel al Jubair: Usiwalaumu wengine kwa hatua zako ghalati

Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika taasisi za kimataifa zenye makao yake mjini Vienna Austria jana usiku alijibu matamshi ya karibuni dhidi ya Iran ya Adel al Jubair Waziri Mshauri Katika Masuala ya Nje wa Saudi Arabia kwa kusema: Iwapo Riyadh inataka kuwa na miradi ya nyuklia au kuibua kisingizio kwa ajili ya kuhalalisha kutoshirikiana na Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Nyuklia (IAEA) basi iwe na uthubutu wa kulipa gharama zake.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Kazem Gharibabadi amebainisha kuwa, ukwamishaji na vitisho ni njia mbili za kawaida zinazotumiwa na waongo na kumhutubu Adel al Jubair kwamba: Usiwalaumu wengine kwa hatua zako ghalati. 

Adel al Jubair Waziri Mshauri Katika Masuala ya Nje wa Saudi Arabia alisema hivi karibuni katika mahojiano kuwa Saudi Arabia itakuwa na haki ya kumiliki silaha za nyuklia iwapo miradi ya nyuklia ya Iran haitasitishwa.

Viongozi wa utawala wa Saudia katika miezi ya karibuni sambamba na viongozi wa utawala wa Kizayuni na Marekani wameibua tuhuma na madai yasiyo na msingi wowote ili kudhihirisha kuwa miradi ya nyuklia ya Iran yenye malengo ya amani ni tishio kwa eneo la Asia Magharibi.  

Madai hayo ya dhihaka ya Saudi Arabia na waitifaki wake yametolewa katika hali ambayo Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) hadi sasa umethibitisha kwa mara kadhaa kupitia ripoti zake juu ya kufungamana Iran na mapatano ya JCPOA na kwamba miradi yake ya nyuklia ni ya malengo ya amani. 

Utawala wa Saudi Arabia umetoa madai hayo huku ikibainika kuwa utawala huo tayari umeanza kurutubisha kwa siri madini ya urani. 

342/