30 Machi 2021 - 12:03
Takht-Ravanchi: Vikwazo vinazidisha mgogoro wa Syria

Mwakilishi wa Kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa ameeleza kuwa, vikwazo vya upande mmoja dhidi ya Syria ni hatua yenye madhara na inayozidisha tu mgogoro wa nchi hiyo na kuwazidishia maumivu wananchi wa nchi hiyo ambayo wanataabika na matatizo mengine mbalimbali kama janga la maambukizi ya corona.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA:Akizungumza jana katika kikao cha Baraza la Usalama la UN kuhusu hali ya kibinadamu ya Syria, Majid Takht- Ravanchi ameongeza kuwa, ripoti ya karibuni ya Katibu Mkuu wa umoja huo kuhusu hatari ya njaa huko Syria katika mwaka huu wa 2021 inatilia mkazo udharura wa kukusanywa haraka iwezekanavyo misaada ya kimataifa kwa ajili ya kukabiliana na changamoto hiyo.  

Ameongeza kuwa, katika hali ambayo kuna udharura wa kufikishwa misaada ya kibinadamu kwa watu wenye uhitaji; kuendelea hali hiyo kwa muda mrefu si tu hakutatui tatizo hilo bali hatua hiyo haiwezi kuwa chaguo mbadala la hatua muhimu zinazopasa kuchukuliwa ili kudhamini usalama, amani na uthabiti wa kudumu huko Syria. 

Mwakilishi wa Iran katika Umoja wa Mataifa amesema kuwa, hatua ya kwanza na muhimu katika uwanja huo ni kudhamini mamlaka kamili ya kujitawala na ya umoja wa ardhi nzima ya Syria kupitia kuwaangamiza magaidi, kuondoka nchini humo wanajeshi vamizi wa nchi ajinabi na kuhitimisha kukaliwa kwa mabavu ardhi ya Syria na kudhamini usalama wa mipaka ya nchi hiyo. 

342/