12 Machi 2022 - 18:39
Mtazamo wa Kiongozi Muadhamu; sisitizo kwa nguvu za taifa na upeo wa mikakati ya Jamhuri ya Kiislamu

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa, nguvu za taifa ni jambo muhimu mno kwa kila nchi na kwamba kila taifa kama linataka kufaidia kweli na uhuru wake, heshima na kustafidi na vyanzo vyake muhimu kwa uhuru na kufanikiwa kusimama imara mbele ya matakwa ya wengine, taifa hilo lazima liwe na nguvu, vinginevyo muda wote litaishi katika udhaifu, udhalili na woga maadamu linahofia tamaa za watu baki.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Ayatullah Sayyid Ali Khamenei alisema hayo jana Alkhamisi wakati aliponana na Mkuu na wajumbe wa Baraza la Wanavyuoni Wataalamu wanaomchagua na kusimamia kazi za Kiongozi Muadhamu na kusema kuwa, mapendekezo kama kulitaka taifa la Iran liache kuwa na ushawishi katika eneo hili ili lisitoe kisingizio kwa adui au kulitaka liachane na maendeleo ya kielimu ya nyuklia, ni pigo kwa nguvu za taifa. 

Amesema: Kuwa na ushawishi katika eneo hili kunatupa upeo mkubwa wa kiistratijia na nguvu zaidi za kitaifa, sasa kwa nini tuachane na jambo hilo? Maendeleo ya kielimu ya nyuklia vile vile yanahusiana na suala la kudhaminiwa mahitaji ya nchi katika mustakbali wa karibuni tu, sasa kama tutaachana nayo, miaka michache baadaye tuje tumnyooshee nani mkono wa kuomba msaada.?

Kina na upeo mkubwa wa kiistratijia wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni suala ambalo Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu amekuwa akilisisitizia mno katika miaka ya hivi karibuni. Maana ya kina na upeo wa kiistratijia inaweza kufafanuliwa kwa sura mbili za hasi na chanya. Kuimarisha usalama na kuondoa vitisho ni katika faida hasi za kina na upeo wa kiistratijia na ni jambo lililo wazi kwamba nchi ambayo ina ushawishi kwa majirani zake, ni mara chache hukumbwa na vitisho na huwa haitoi gharama kubwa katika kudhamini usalama wa eneo linaloizunguka.

342/