Kwa mujibu wa shirika la habari la Riannosti, Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia, Sergei Lavrov, amesema hayo mbele ya waandishi wa habari akiwa pamoja na mwenyeji wake, Waziri wa Mambo ya Nje wa Burkina faso na kusisitiza kuwa, uhusiano wa Moscow na Ouagadougou unazidi kuimarika katika uwanja wa kijeshi na kiufundi.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia pia amesema kuwa, nchi yake ina nia ya kupeleka zana zaidi za kijeshi nchini Burkina Faso ili kuimarisha uwezo wake wa ulinzi. Ziara hiyo ya Lavrov imekuja baada ya ile ya Naibu Waziri wa Ulinzi wa wa Russia aliyetembelea Burkina Faso Juni 4 na kutangaza kuwa wakufunzi wa kijeshi wa Russia wataongezwa nchini humo.
Lavrov aliwasili katika Uwanja wa Ndege wa Ouagadougou mji mkuu wa Burkina Faso akitokea Kongo.
Alikaribishwa na Karamoko Jean Marie Traore, Waziri wa Mambo ya Nje wa Burkina Faso katika uwanja wa ndege wa Ouagadougou.
Lavrov alianza ziara yake ya kuzitembelea nchi kadhaa za Afrika siku ya Jumatatu.
342/